Skip to main content

Posts

MAKOMBENI WAOMBA KUONGEZEWA DOZI ATHARI UTIRIRISHAJI MAJI TAKA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Makombeni wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema bado wanahitaji elimu zaidi ya athari za utiririshaji maji machafu katika makaazi yao, ili kujiepusha na magonjwa ya kuharisha na kutapika. Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika shehiani hapo, walisema bado wapo baadhi yao wamekuwa wakitiririshaji maji hayo, bila ya kujalia afya za wenzao. Walieleza kuw, inawezekana wanaofanya jambo hilo ni kutokujua athari za maji hayo kwa jamii na hasa watoto ambao tahadhari yao ni ndogo. Mmoja kati ya wananchi hao Ali Khamis Juma alisema, moja ya chanzo cha utirirshaji wa maji hayo, ni magonjwa kama ya tumbo la kuharakisha na kutapika. ‘’Ni kweli suala la uchafuzi wa mazingira hasa la utiririshaji maji machafu lipo kwenye shehia yetu, na inawezekana wengi wao hawajui madhara,’’alieleza. Nae Semeni Juma Kheir, alisema hayo yanajitokeza kutokana na kutokuwepo kwa adhabu kali kwa wananchi wanaodharau uchimbaji wa shimo la kuhifadhi maji ...

‘KINJE KUKU’ UTAMADUNI WA MICHEWENI UNAOWAHUSU WATOTO WA KIKE PEKEE

  NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ UTAMADUNI wa uvaaji kanga ya shingoni, ama kwa lugha Micheweni ‘kinje kuku’ umepotea kwa kasi. Kizazi cha sasa cha Micheweni, na hasa watoto wa kike ambao ndio walengwa wa utamaduni, wameanza kuupa kisigo. Wakionekana, kuachana na vazi hilo, na sasa wakivaa nguo nyingine ambazo wanaona zinawastiri hasa sehemu ya kifuani.   Hiyo ni kutokana na karne ya sasa na utandawazi jinsi ulivyokua, ndipo watoto wa kike wa Micheweni takribani kwa asilimia kubwa kuacha utamaduni huo. Vazi hili lilikua linavaliwa sana na watoto, wengi wao wanaishi vijijini, lengo hasa la kinje kuku, ni kuwastiri watoto hao wa kike sehemu ya kifuani, hasa wakianza kutanuka kifua. Vipo vijiji vyengine vingi katika Mkoa huo   ambavyo watoto wa kike walikua wanavaa vazi hilo kama utamaduni wao, lakini mwandishi wa makala hii aliamua kwenda kwenye kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni kuzungumza na wazee.   Wilaya ya Micheweni ni Mkoa unaoongoza kwa masuala ...

WASIOJULIKANA WAIBA MAZAO YA BAHARINI MTAMBWE PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATU wasiojulikana, wamevamia na kuiba Kaa na Vitango bahari, waliyokuwa yakifugwa na wanaushirika wa ‘yashasemwa’ uliopo shehia ya Mtambwe kusini, wilaya ya Wete Pemba. Watu hao kwa nyakati tofauti, wanadaiwa kuiba Kaa 80 kati ya 120 waliyoyaingiza na Vitango bahari kuibiwa yote 1,000 kwa nyakati za usiku.   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, viongozi wa ushirik huo, walisema wizi huo umefanyika miezi mitano, baada ya kuweka vifaranga hivyo, kwa ajili ya ufugaji. Msaidizi wa Mwenyekiti wa ushirika huo Jabir Saleh Jabir, wamepatwa na mshangao mkubwa, baada ya kupokea taarifa za kuibiwa, kwenye shamba lao. Alisema, walitumia gharama kubwa kuanzisha maeneo hayo husika, kwa ajili ya ufugaji wa vitango bahari na Kaa, ingawa watu wasiowafahamu, waliwarejesha nyuma kwa kuwaibia. ‘’Na sisi ni ushirika ambao tuna nia ya kuvuna matunda ya uchumi wa buluu, na tulishajikusanya na kuunganisha nguvu zetu, lakini wengine waliamua kuturejesha ...

MWENGE WA UHURU WATUA PEMBA, WAANZA WILAYA YA WETE UFUNGUZI WA MIRADI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWENGE wa uhuru umewasili kisiwani Pemba, ukitokea Mkoa wa kaskazini Unguja, tayari kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya nne za Pemba, samba mba na ufunguzi wa miradi kadhaa, ikiwemo ya maendeleo kisiwani humo. Mwenge huo umepokelewa jana, katika uwanja wa ndege wa Karume Pemba, ambapo wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, wamejumuika. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahamoud, alisema mwenge huo ukiwa mkoa mwake, ulizindua miradi minane ya maendeleo na program nne, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 14.4. Alisema wakimbiza mwenge, walitoa ujumbe kwa wananchi, ukiwemo suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira, lishe na kupinga rushwa na kisha kuchunguza afya kwa wananchi. Mkuu huyo wa Mkoa, alisema katika kipindi hichi, walipanda miti 120,000, ingawa katika shamra shamra za mwenge wamepanda miti 2,500. ‘’Mkuu wa mkoa wa...

WAZAZI, WALEZI WAWAPA TANO WAALIMU CONNECTING, KAZI IENDELEE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZAZI na walezi wenye watoto wao skuli ya sekondari ya Connecting Continent ya Mgogoni wilaya ya Chake chake, wamesema wameridhishwa na juhudi binafsi za waalimu, katika kuwafundisha wanafunzi skulini hapo. Wakizungumza kwenye mkutano maalum uliofanyika skulini hapo, wenye lengo la kupokea matokeo ya muhula wa kwanza, wazazi na walezi hao, walisema kutokana na ugumu wa wanafunzi ulivyo, wanaridhishwa na juhudi zao. Walisema, wengi wao wamekuwa wakikosa muda wa kuwauliza watoto wao juu ya maendeleo ya elimu, lakini waalimu hao, wamekuwa wakibuni mbinu za kuwaendeleza wanafunzi. Wazazi hao walieleza kuwa, kwa muhula huu kwanza, wameridhishwa na matokeo hayo, ambayo kwa yale ya darasa la 12, kama yengekuwa ndio ya mitihani ya taifa, kusingekuwa na mwanafunzi aliyefeli. Mmoja kati ya wazazi hao Omar Mjaka Ali, alisema kama sio juhudi za waalimu hao na mbinu mbali mbali za kuwalazimisha wanafunzi kusoma, matokeo ya muhula wa kwanza, yasingekuwa maz...

WADAU: ‘WAHANGA WA UDHALILISHAJI WALIPWE FIDIA ZAO

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA “NILIAMBIWA mahkamani kua, mtoto wangu atalipwa shilingi milioni 1 ya fidia, tangu mwaka jana, mshitakiwa alipotiwa hatiani, lakini sasa ni miaka miwili hajapewa, mpaka mshitakiwa alipoondolewa hukumu kwa madai ya ugonjwa wa akili,’’anasema mzazi mmoja. Mama huyo mkaazi wa Wingwi Wilaya ya Micheweni ambae mtoto wake wa miaka mitatu (3) alifanyiwa kitendo cha ubakaji na kijana wa miaka zaidi ya 28. Anaeleza kuwa, alitegemea fedha hizo zitamsaidia kumshughulikia mtoto wake ambae aliathirika kisaikologia na kimwili, ingawa hajaulizwa chochote tangu kesi hiyo ilipopata hukumu mwaka jana. “Kinachoniumiza zaidi ni kuona yule mshitakiwa alitakiwa kutumikia chuo cha mafunzo miaka 30, lakini haijatimia mwaka, ameshatolewa eti kwa madai kuwa ni mgonjwa wa akili, na amekwenda Unguja Mental”, anaeleza. Anasema kijana huyo hajawahi kumuona wala kusikia kwamba ana ugonjwa wa akili, isipokuwa wanafanya hivyo ili asifungwe wala alimlipe fidia. Mama huyo sio pe...

WANAWAKE WANAOZALISHA BIDHAA ZA CHAZA LULU MAKOMBENI WALA HASARA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAUSHIRIKA wa ‘tujikombowe’ wa shehia ya Mkombeni wilaya ya Mkoani Pemba, unaojisghulisha na ufugaji wa chaza lulu, wamepata hasara ya zaidi ya shilingi 600,000 baada ya bidhaa zitokanazo na rasilimali hiyo, kukosa wateja. Bidhaa hizo aina herini pea 25, ambazo moja ni shilingi 25,000 wamelazimika kuzibakisha ofisini kwao, baada ya kukosa wateja kwa muda mrefu sasa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema awali walikuwa na changamoto ya ukosefu wa mashine ya kusarifia bidhaa hizo, ingawa baada ya kuipata sasa changamoto ni soko la bidhaa hizo. Walisema, kwa mara ya kwanza walizalisha herini hizo na kuziuza kwa thamani ya shilingi 300,000 ingawa kwa msimu mwengine walikosa wateja wa bidhaa hizo. Mwenyekiti wa ushirika huo Faida Faki Kombo, alisema kwa sasa hawajui herini hizo pea 25 wazifanye nini bali wanachoshuhudia ni kuendelea kuchakaa na kupoteza thamani. Alieleza kuwa, soko la wateja wao kwa sasa limepotea na kusababisha kup...

SKULI MPYA YA GHOROFA MWAMBE, KUPUNGUZA UFINYU WA NAFASI KWA WANAFUNZI?

      NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ILIKUA kama ndoto, kwa siku ya kwanza kati ya zile 360 zinazounda mwaka, kwa waalimu, wanafunzi, wazazi, walezi wa Mwambe, kunawa uso mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi. Sio tu kunawa uso, kwa maji kama ilivyozeeleka, wao walinawa kwa kumalizika skuli ya msingi ya ghorofa mbili eneo hilo la Mwambe. Hapa wazazi, walezi, wanafunzi na waalimu, maji kwenye upindo wa kucha ya mtoto mchanga, yalitosha kuwakogesha mwili mzima. Furaha yao, sio tu kuamka wakiwa wazima siku hiyo ya Januari 1, mwaka 2023, lakini ni pale waliposhuhudia jengo la kwanza la ghorofa katika eneo la Mwambe, na bahati nzuri sio la mtu binafsi, bali likiwa la serikali. WANANCHI MWAMBE Haji Omar Kheir, anasema aliposikia ahadi ya rais wa sasa wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, juu ya ujenzi wa skuli ya ghorofa, hakuamini akilini mwake. ‘’Si unajua baadhi ya wanasiasa wakitaka jambo lao, watakuahidi jambo hata...