Skip to main content

Posts

KUNDI LA VIIZIWI LIANZE SASA KUTENGENEZEWA MAZINGIRA YA KUPATA TAARIFA UCHAGUZI MKUU UJAO

                                                                 PICHA NA MTANDAO SIO HALISI YA VIZIWI NA HAJI NASSOR, PEMBA ULEMAVU ni upungufu wa uwezo wa viungo vya mwili, akili au hisi unaomsababishia mtu, kushindwa kumudu mazingira yake au kushindwa kushiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Ndivyo ilivyoa toa tafsiri ya nini maana ya ulemavu, sheria ya watu wenye ulemavu (haki na fursa ) ile namba 9 ya mwaka 2006 ya Zanzibar ielezavyo. Sheria hii ikaenda mbali zaidi na kufafanua kuwa, ulemavu unaweza kuwa wa kudumu au wakati mwengine ni wa muda, huku baadhi ya magonjwa kama vile ya akili yanaweza kusababisha ulemavu pia. Tendo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutunga sheria hii, ni kuona umuhimu na ulazimu ule uliomo kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwamba binadamu wote ni  sawa mbele ya sheria. Kumb...

WANANCHI MFIKIWA CHAKE CHAKE: MRADI WA DUMISHA AMANI UMEPUNGUZA MISUGUANO

    HABIBA ZARALI, PEMBA   WANANCHI wa shehia ya Mfikiwa Wilaya ya Chake chake kisiwani Pemba, wameupongeza mradi wa 'dumisha amani Zanzibar’ kwa kuwapa elimu ya utatuzi wa migogoro, uliowawezesha kupunguza mivutano na sasa kuishi kwa amani.   Walisema kabla ya kuwafikiwa na mradi huo, katika shehia yao kulikithiri migogoro hasa ya ardhi, kati yao na serikali ingawa kwa sasa hali inaendelea vizuri.   Wakizungumza kwenye mkutano wa ufupisho wa mradi huo na kuangalia changamoto za migogoro, waliyoibuwa ulioandaliwa na tasisi ya Search for Common Ground na Foundation for civil society shehiani humo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo walisema chanzo cha uvunjifu wa amani ni kutotendeka kwa haki.   Mmoja kati ya wananchi hao Khamis Ali Khamis, alisema migogoro ya ardhi, waliyokuwa nayo nyuma ilisababishwa na kutotendewa haki na baadhi ya taasisi za serikai, baada ya kuchukuwa ardhi bila ya kuwashirikisha wananchi.   Alisem...

TAMWA ZANZIBAR YATAKA UWEPO MAZINGIRA YA USAWA WA KUJINSIA ZEC

  MUHAMMED KHAMIS, TAMWA- ZNZ:: CHAMA cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar kimesema  wakati umefika kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar 'ZEC' kuhakikisha kinaweka mazingira ya usawa wa kijinsia, katika utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali, zikiwemo za usimamizi wa chaguzi na nyenginezo.   Kauli hiyo  imekuja  kufuatia mkutano malumu wa majadiliano, baada ya  kumalizika kwa mkutano  awali uliofanyika Septemba mwaka jana na kupeana na majukumu kwa pande zote mbili kupitia, sera jinsia ya mjumuisho kwa ajili ya kutazama uwepo wa mazingira ya  usawa wa kijinsia katika muundo wa tume hiyo na utendaji wa kazi zake.   Akizunguma katika mkutano huo Mkurugenzi wa Chama hicho Dk.Mzuri alisema ushiriki wa wanawake katika shuhuli za tume hiyo utaleta mwanga zaidi na hatikame kuwafanya wanawake wengi waweze kufikia malengo yao yakiwemo ya kuwa viongozi.   Alisema kwa miaka mingi katika kazi za tume hiyo kumeonekana  wanaume weng...

MISA: WAANDISHI ZIELIMISHENI MAMLAKA UMUHIMU WA SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR

  NA HAJI NASSOR. UNGUJA WAANDISHI wa habari Zanzibar, wamesisitizwa kuendelea kuzielimisha mamlaka za nchi, juu ya umuhimu wa kuwa na sheria rafiki za habari kwa maendeleo ya taifa. Ushauri huo umetolewa na mataalum wa sheria Tanzania Chris Maina Peter, wakati akiwasilisha sheria zinazosimamia habari Zanzibar, kwenye mkutano wa siku moja, ulioandaliwa na Tasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA- Tanzania na kufanyika hotel ya Golden Tulip uwanja wa ndege Unguja juzi August, 22, mwaka 2022. Alisema moja ya jukumu la vyombo vya habari, ni kutumia kalamu zao vyema kwa kuielimisha jamii na mamlaka husika kuelekea mabadiliko ya sheria. Alieleza kuwa inawezekana mamlaka za nchi hazielewi ubaya na athari zilizopo katika tansia ya habari, hivyo wakiwaeleza wanaweza kuona. "Jengine umoja na mshikamano wa hali ya juu ikiwa mbona mnasheria inakwaza kazi zenu ili mziambie mamlaka juu ya marekebisho hayo,"alieleza. Katika hatua nyingine Professa  Chris, alisema nchi inapokuwa n...

ITATUENI MIGOGORO YA MADAI MSIKIMBILIE MAHAKAMANI: SEARCH

  JAMII Kisiwani Pemba, imetakiwa kuwa na mwamko wa kujua kuwa, jukumu la utatuzi wa migogoro kwa makosa ya madai, kwa njia ya amani ni lao wenyewe kabla ya kufika katika vyombo vya sheria. Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa taasisi ya foundation for civil society Khamis Abass katika kikao cha kubadilishana mawazo, na kuandaa mikakati itakayosaidia kuondowa changamoto zilizojitokeza katika hatuwa za awali za utekelezaji wa mradi wa 'Dumisha amani Zanzibar' kilichofanyika shehia ya Ngwachani Wilaya ya Mkoani Pemba. Alisema katika utekelezaji wa mradi huo kumeweza kuibuliwa migogoro mingi ikiwemo ya ardhi, ndoa, siasa, na mengine ambayo inaweza kusuluhishwa kwa kukaa pamoja wanajamii wenyewe. Alifahamisha kuwa, ukosefu wa amani unatokea baada ya jamii kutokuwa na mazungumzo ya pamoja pale baada ya kutokezea migogoro hasa yale ya madai. "Iwapo jamii itaipa nafasi migogoro kutawala ni wazi kuwa amani itakuwa tunu na wakati huohuo shughuli za kimaendeleo ziakosekana",a...

WATAALAMU ECD PEMBA WATAJA ATHARI ZA KUINGILIA FARAGHA MTOTO

  NA HAJI NASSOR,  PEMBA WAZAZI na walezi visiwani Zanzibar, wametakiwa kutoingilia kimabavu, faragha za watoto wao, kwani kufanya hivyo, kunaweza kuwa chanzo cha ukosefu wa nidhamu kwao, katika maisha yao ya baadae. Ushauri huo umetolewa na wataalamu wa malezi na makuzi ya kisayansi ya awali ya watoto ‘SECD’ kisiwani Pemba, wakati wakizungumza na mwandishi wa habari, juu ya dhana ya faragha kwa watoto wadogo. Walisema, suala la faragha na umri wa mwanadamu halina uhusiano wowote, hivyo watoto kama walivyo watu wazima, hawatakiwi kubugudhiwa na kuingiliwa kimabavu faragha zao. Mmoja kati ya wataalamu hao, Rashid Said Nassor, alisema faragha hata ya mtoto mdogo, mzazi, mlezi au mtu mwengine, hatakiwi kuiingilia, kwani kufanya hivyo ni kumvunjia haki zake. Alieleza kuwa, mtoto ni mwanadamu kama walivyo wengine, hivyo anaowakati hujiweka kwenye faragha yake, na kufanya mambo yake binafsi, na mzazi au malezi hatakiwa kumyima uhuru huo. ‘’Mtumzima gani ambae ana...

NAIBU WAZIRI MAJI ZANZIBAR ASEMA YUKO TAYARI KUONESWA NJIA

  Na Salma Lusangi  NAIBU  waziri Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar  Shabaan Ali Othman amesema uongozi wa wizara yake uko tayari kukosolewa pamoja  na kupokea maelekezo yaliyotolewa na kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ili kuleta ufanisi katika  majukumu ya  wizara hiyo.   Akizungumza katika kikao cha majumuisho kilichofanyika  jana katika ukumbi wa ZURA Maisara Zanzibar, baada ya kamati hiyo kumaliza ziara ya  kutembelea miradi ya umeme na maji kwa Unguja na Pemba ambayo  inatekelezwa na  WMNM, alisema wapo tayari kukosolewa kiutendaji  pamoja na kupokea ushauri ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia  wananchi.   “Kwanza nawapongeza watendaji wote hasa nampongeza Katibu Mkuu Kilangi, kama wizara tumepokea maelekezo ya kamati,tutayatekeleza kama tulivyotumwa naomba kamati  isisite kutukosoa  zaidi naona kamati imetoa ushauri mzuri utatusaidia sana k...

MWALIMU SKULI YA MADUNGU KUPANDISHWA MAHAKAMANI PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: JESHI la Polisi mkoa wa kusini Pemba, litampandisha mahakamani wakati wowote, Mwalimu skuli ya Msingi ya Madungu wilaya ya Chake chake Pemba, Ali Makame Khatib, akidaiwa kumchezea sehemu zake za siri na kisha kumbaka, mwanafunzi wake wa darasa la tano skuli hapo. Taarifa za Jeshi hilo, zilizotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo, Abdalla Hussein Mussa alisema, kwa sasa wanaendelea kumuhoji mwalimu huyo, kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, na kisha taratibu zikikamalika atafikishwa mahakamani. Alieleza kuwa, awali walipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo, akidai mtoto wake, amechezewa na kisha kuingiliwa na mwalimu wake. Kamanda huyo alieleza kuwa, baadae taratibu za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, zilifuata na kuanza kuhojiwa juu ya tuhuma hizo. Awali mama mzazi alidai kuwa, aligundua tatizo hilo kwa mtoto wake, baada ya kusikiliza moja ya kituo cha redio kikielezea aina za udhalilishaji. Mama huyo alieleza kuwa, mtoto wake ...

WIZARA YATILIANA SAINI NA 'GWP' KUONDOA SHIDA YA MAJI ZANZIBAR

  NA SALMA LUSANGI, WMNM-ZANZIBAR::: WIZARA ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, imetiliana saini ya makubaliano (MoU)  na taasisi ya 'Global Water Partnership (GWP)'  kuhusu utekelezaji wa mpango mkuu wa maji safi na salama Zanzibar. Hafla hiyo ya kutiliana saini imefanyika mjini, Zanzibar baina ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Joseph Kilangi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya GWP Dk. Victor Kongo na  kushuhudiwa na viongozi wakuu na watendaji wa taasisi mbili hizo.     Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Katibu Mkuu huyo alisema kupitia makubaliano hayo Mpango Mkuu wa Maji Zanzibar wa mwaka 2022/2027 utaweza kutekelezeka kwa haraka na kuleta ufanisi ambao Wizara yake inahitaji katika utekelezaji wa huduma ya maji  Zanzibar. Alisema  changamoto zilizopo katika masuala ya maji yanahitaji utafiti wa kina ikiwemo miundombinu ya maji, maeneo sahihi ya kuchimba visima na mambo mengine ya kitalaamu ili Wizara yake iweze  kutatua tatizo la maji ...