IMEANDIKWA NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ WANANCHI wametakiwa kuwatumia wasaidizi wa Sheria waliomo shehiani mwao, ili kupatiwa msaada wa kisheria kwalengo la kupata haki zao za msingi. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala bora Zanzibar Salma Suleiman wakati akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Msuka, katika mkutano maalumu wa kuijengea uwelewa jamii juu ya masuala ya kisheria, uliofanyika Skuli ya Sekondari Msuka wilaya yaMicheweni Kaskazini Pemba. Alisema Wananchi waliowengi wamekua wakipata matatizo mbali mbali ikiwemo migogoro ya ndoa, Ardhi pamoja na utelekezwaji, lakini bado uwelewa wa kuwatumia wasaidizi wa Sheria katika kuzitatua changamoto hiyo. Alisema kazi kubwa ya Wasaidizi wa Sheria ni kuhakikisha wanatoa msaada wa kisheria katika Jamii, hivyo ni mihimu kwa jamii kuwatumia wasaidizi hao, ili kupata ufumbuzi wa changamoto. ‘’Wasaidizi wa Sheria ni watu ambao wanatambulika kisheria, hivyo watumien...