Skip to main content

Posts

KAMATI YA MAADILI YAPIGA MARUFUKU 'BEACH' YA WAMBAA KUGEUZWA 'GEST BUBU'

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KAMATI ya maadili na taaluma ya shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, imepiga marufuku kufanyika vitendo viovu, vinavyofanywa na baadhi ya vijana, katika ya fukwe ya bandari ya Kwakitunga Wambaa. Kamati hiyo imesema, wamebaini kuwa, kila ifikapo siku za sikukuu na mwishoni mwa wiki, wapo vijana, wengi wao kutoka nje ya shehia hizo, huitumia fukwe hiyo, kwa kufanya mambo machafu. Akizungumza kwenye kongamano la malezi na maadili, lililofanyika Wambaa sokoni, Mjumbe wa kamati hiyo sheikhe Mahamoud Hussein, alisema hawakatai vijana kusherehekea sikukuu, bali wanachopiga marufuku ni uvunjifu wa maadili. Alisema, suala la furaha ni jambo jema, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan, ingawa wanachokipinga ni kufanyikwa vitendo vya udhalilishaji. Alieleza kuwa, uislamu haukatazi furaha kwa mtu yeyote, bali kinachotakiwa iwe ni kwa kufuata maadili na misingi ya dini ya kiislamu, ili furaha hiyo isigeuke nakama. ‘’Kama...

TIMU YA MPIRA WA PETE YA WANAWAKE MCHANGA MDOGO YATAKA LIGI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@  WACHEZAJI wa timu ya mchezo wa Pete ya Wanawake ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete, wamesema wanatamani kushiriki, ligi kuu ya mchezo huo, ili kukuza vipaji vyao. Walisema, wameamua kuchagua kuanzisha timu ya mchezo huo, wakiamini kuwa wanaweza kusonga mbele kwenye eneo hilo kupitia ligi kuu ya Zanzibar, itayoanzishwa. Hayo yameelezwa na wachezaji na viongozi wa klabu hiyo leo Machi 24, mwaka huu wakati wakizungumza na waandishi wa habari, kufuatilia tathmini ya mafanikio ya mradi wa ‘’michezo kwa maendeleo,’’uliokuwa ukitekelezwa na TAMWA, ZAFELA na CYD. Walisema, baada ya kupewa mafunzo na TAMWA ya umuhimu wa kushiriki kwenye michezo, kwa maendeleo wamehamasika kuanzisha timu ya mchezo wa pete. Walisema, wanazotaarifa kuwa, kwa upande wa Pemba, mchezo huo haujawahi kuanzishiwa ligi kuu, iwe ngazi ya wilaya au mkoa, jambo linalotishia ndoto zao. Mchezaji wa timu hiyo Zainab Rashid Said, amesema ni wakati sasa kwa viongozi kuhakikisha ligi ya m...

DC MKOANI MGENI RASMI MASHINDANI TAHAFIDH QUR-AN WAMBAA

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ MKUU wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, kesho  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika mashindani ya tano ya tahafidhil-quran, ya kanda ya Wambaa wilayani humo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa Jumuiya ya tahafidhil qur-an kanda ya Wambaa, Mwalimu Abdalla Haji Ali, alisema tayari maandalizi ya shughuli hiyo, yameshakamilika. Alisema, mkuu huyo wa wilaya, atawashuhudia wanafunzi wakishindana kwa juzuu ya kwanza, pili, tatu, tano, saba, 10 na 15 wakiwemo wanafunzi wa kike na kiume. Alieleza kuwa, mashindani hayo ya aina yake kwa mwaka huu, yanatarajiwa kufanyika msikiti wa Ijumaa, uliopo kijiji cha Chumbageni Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba. Alisema, baada ya majaji kukamilisha kazi yao hiyo na kutoa matokeo, mgeni rasmi huyo atatoa zawadi ikiwemo fedha taslimu, kwa washindi na washiriki wote 42. ‘’Ni kweli asubuhi hii, ndani ya msikiti wa Ijumaa Chumbageni, mkuu wetu wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, atayashuhudia mashindani y...

MJAKA`S LESSON: STRENGTH IN SUPPORTING WOMEN

  BY KHELEF NASSOR, ZANZIBAR@@@ Mjaka Faki Ali, a father of four from Kiuyu Minungwini, North Pemba, is breaking barriers and rewriting the narrative of gender equality and environmental conservation. He is a husband who proves that his wife’s success is the success of the entire family. Mjaka is the husband of Sada Faki Jabu, a resilient woman driven by the dream of becoming a leader in the fight against climate change. Through the Zanzibar Women Leadership in Adaptation (ZanzADAPT) project , funded by the Global Affairs Canada and implemented by Community Forests Pemba in collaboration with Community Forests International , Sada has received training in agroforestry , a sustainable farming method that preserves the environment while ensuring food security for families and communities. Unlike many men who perceive farming as solely their wives' responsibility, Mjaka saw his wife’s agricultural efforts as a shared journey. “I chose to support my wife because I want her to ...

RC SALAMA: ASEMA JAMBO KUHUSU ZSSF, MASHEHA KASKAZINI PEMBA

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ MKUU wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib amesema vikao kazi kwa masheha na watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ‘ZSSF’ vinasaidia kuongeza ushirikiano na ufanisi wa kazi. Alisema, unapokuwa karibu na ofisi ya tawala za Mikoa ndio umeifikia jamii kwa urahisi, na kiyume chake ni kudhoofisha utendaji kazi ofisi isiyotaka ushirikiano na masheha. Hayo yameelezwa leo Machi 7, 2025 na Mkuu wa wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali, kupitia hutuba ya Mkuu huyo mkoa, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi, cha masheha na watendaji wa ZSSF, kilichofanyika ukumbi wa mikutano Jamhuri Wete. Alisema, ushirikiano huo ambao ‘ZSSF’ wameuomba ni eneo zuri la utendaji kazi, kwani chanzo cha jamii na kuifikia kwa haraka na wepesi ni uwepo wa masheha. Alieleza kuwa, kilichofanywa na ‘ZSSF’ kinaashiria umoja na mshikamo katika kufanikisha majukumu ya kila siku, yanayosimamiwa na viongozi wakuu wa nchi. Alifahamisha kuwa, ndani ya wilaya na mkoa, wamekuwa...

ZSSF: 'MASHEHA WARIPOTINI WANACHAMA WETU WANAOFARIKI KUONDOA UDANGANYIFU'

    N A FATMA HAMAD , PEMBA@@@@ MASHEHA wa mkoani wa kusini Pemba, wametakiwa kutoa taarifa kwa  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ,  endapo kutatokea  kifo cha mwanachama wa mfuko huo katika shehia zao, ili kupunguza udanganyifu hasa katika malipo ya fedha za s erikali. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mafao kutoka Mfuko huo Zanzibar, Mussa Yussuf wakati akiwasilisha mada ya dhima ya m asheha ,  katika utoaji wa huduma za ZSSF ,  k wenye kikao kazi kilichofanyika leo Machi 6, 2025 Tibirinzi Chakechake Pemba. Alisema kumekuwepo na baadhi ya watu wamekua wakipeleka taairifa za vifo vya jamaa zao  katika mfuko huo ,  ambazo si o  za ukweli, hivyo endapo watapeleka taarifa wataepusha kutokea kwa udanganyifu  huo . ‘’Wamekua wakitujia watu na taarifa za jamaa zao kufariki na kudai mafao yao, lakini tukifanya uchunguzi tunagundua kwamba sio ukweli ni uzushi  mtupu, hivyo mtusaidie ,’’alisema. Ali fafanua  kuwa ,  endapo M...

WASTAAFU WATARAJIWA PEMBA WANOLEWA KUYAKABILI MAISHA YA URAIANI

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WATUMISHI wa umma wanaotarajiwa kustaafu wametakiwa kuwa makini wanapopokea ushauri wa watu mbali mbali, ili waepuke kupoteza fedha nyingi bila ya mafanikio. Akifungua mafunzo kwa wastaafu hao watarajiwa, leo Machi 5, mwaka 2025 Afisa Mdhamin Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali alisema, kuna watu wengi watajitokeza kuwapa ushauri wa mambo mbali mbali, hivyo wawe makini katika kuupokea na kuutekeleza. Alisema kuwa, wastaafu bado wana mchango mkubwa kwa taifa, hivyo kuna haja ya kujipanga mapema katika kujitafutia miradi ambayo itaendeleza maisha yao baada ya kustaafu. "Kila mtu atakujia kukushauri kufanya biashara na wingine watakushauri kufanya vitu vyingine, lakini muwe makini ili fedha zenu za kiinua mgongo, zitumike kuwakomboa kimaisha na sio kuwasababishia matatizo," alisema Mdhamini huyo. Aliwataka watumishi hao wayafanyie kazi mafunzo waliyopatiwa, kwani wanakwenda kulitumikia taifa kwa upande mwingin...

VIJANA WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

IMEANDIKWA NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@ MKAGUZI wa shehia ya Pandani Wilaya ya Wete Pemba, Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi amewataka vijana kufanya kazi za kuwapatia kipato ili kuepukana na vitendo viovu, ambavyo ni hatarishi na vinaweza kuharibu malengo yao. Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi viatu Sultan Hamad Issa ambaye ni mjasirimali mwenye mlemavu wa ngozi mkaazi wa shehia ya Pandani wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema, kuna baadhi ya vijana wenye ulemavu wanashindwa kujishughulisha na badala yake kutegemea wazee, jambo ambalo linaongeza mzigo katika familia, kwani ulemavu mwengine unamuwezesha kijana kufanya kazi na kuweza kujikwamua kiuchumi. ‘’Nampongeza kijana huyu kwa kushirikiana na wenzake na kujiajiri kwa kuanzisha kikundi cha mifugo, ili kuweza kupata za mkopo, mafunzo na kitendea kazi ambavyo vinaweza kuboresha mradi wao,’’ alisema Mkaguzi huyo. Aidha, alimpongeza kijana huyo kwa kuamua kushirikiana na wenzake katika...

ZULEKHA’S JOURNEY: FROM STRUGGLES TO LEADERSHIP IN CLIMATE-RESILIENT AGROFORESTRY

  BY KHELEF NASSOR, ZANZIBAR@@@ Zulekha Ali Mohammed, a 26-year-old woman from Hindi village in Kambini Shehia, Wete District, Pemba, has emerged as a beacon of hope for many women in her community. Born in Wingwi village, Micheweni District, she grew up in a rural setting where access to higher education was a challenge for many girls. After completing her secondary education at Wingwi Secondary School in 2013, she remained at home, assisting her parents in farming. In 2015, Zulekha was forced into marriage, and over the years, she became a mother to five children—two boys and three girls. Like many rural women, she found herself in an extended family setup, struggling to meet household expenses. Determined to support her husband and ensure food security for her children, she joined him in farming. However, the journey was far from easy. “We spent many hours working on our farm, but because we lacked modern agricultural skills and relied on traditional farming methods, our har...