Skip to main content

Posts

WANANCHI TIRONI WATAMANI BARABARA YA LAMI, WIZARA YATIA NENO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa vijiji vya Tironi na Kionwa, wilaya ya Mkoani Pemba, wameikumbusha wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, kuwafikiria ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha lami, iliyoanzia Mbunguwani. Walisema, wanaona wivu mkubwa kuona zipo barabara za ndani, kwa sasa zinaendelea na ujenzi, ambao yao haijaanza hata kupimwa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema wakati umefika kwa sasa, kwa wizara husika, kuwatupia jicho, ili waondokane na usumbufu hasa kipincdi cha mvua. Walisema, barabara yao imekuwa ikitoa kwa wingi zao la taifa la karafuu, hivyo ni vyema sasa mapato ya nchi hii, yakaelekezwa kwao, kwa ujenzi wa barabara yao. Mmoja kati ya wananchi hao Maryam Haji Khamis, alisema wamekuwa wakipata dhiki, hasa wanapopata uhamisho wa kimatibabu. ‘’Kwa mfano sisi wazazi, wakati mwingine tunahitajika kwenda kirufaa hospitali ya wilaya ya Mkoani, lakini usumbufu, ni uwepo wa barabara iliyochakaa,’’alieleza...

MRADI 'URAIA WETU' PEMBA, WAIBUA RUNDO LA CHANGAMOTO ZA KISHERIA, SERA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWEMVULI wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ umekutana na wadau wake, ili kuibua changamoto za kisheria na kisera, zinazotajwa kurejesha nyuma, utendaji wa kazi zao na jamii kwa ujumla. Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika leo Novemba 3, 2024 ukumbi wa Maktaba Chake chake, Katibu Mkuu wa ‘PACSO’ Sifuni Ali Haji, alisema lengo la mkutano huo, ni kuibua changamoto hizo na kuzifanyia kazi. Alisema, ‘PACSO’ kwa sasa inaendelea na utekelezaji wa mradi wa urai wetu, ambapo moja ya eneo la utekelezaji wake, ni kuibua changamoto za kisheria na sera, zinazokwaza makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Alieleza kuwa, changamoto hizo kisha, huziwasilisha kwa jumuia pacha wanaotekeleza mradi huo pamoja, ambayo ni Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAUZA’. Katibu Mkuu huyo alifahamisha kuwa, mfano wa jambo kama hilo, tayari zipo changamoto ambazo awali ya mwaka huu, ziliibuliwa na ‘PACSO’ na kuzifikisha kwa ‘JUWAUZA’ kwa hatua ya ...

WEMA: YATOA TAHADHARI WANAOSUBIRI AJIRA ZA UALIMU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imewatahadharisha wazazi, walezi na vijana wanaosubiri ajira za uwalimu, kuwa makini kwani, kwani matapeli wanaweza kuingilia kati zoezi hilo. Wizara hiyo imesema, matapeli wanaweza kuwahadaa wazazi, walezi au wataka ajaira hizo, na kuanza kuwapa maelekezo mingine yasiokuwa au yanayofafana na ya wizara, ili kuwatoleshea fedha. Akizungumza na waandishi wa habari Pemba, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said, alisema ni kweli, katika mwaka huu wa fedha, wizra inaompango wa kuajiri waalimu, lakini nao matapeli wanaweza kutumia fursa hiyo. Alieleza kuwa, ndio maana wizara imeona iwatahadharishe wazazi na vijana wenyewe mapema, ili zoezi litakapoanza lisije kuwaathiri wananchi. Katibu mkuu huyo alieleza kuwa, maana wakati huo wa zoezi likiwa katika mchakato, wapo wanaoonekana kulalamikiwa, baada ya kupigiwa simu wakiahidiwa kusaidiwa kupata ajira hizo. ‘’Wizara ya Elim una Mafunzo ya Amali, i...

HATIMAE BARABARA MELI TANO- WETE YAANZA KUTIWA LAMI, WANANCHI HAWAAMINI MACHO YAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI na waendesha vyombo vya moto wanaotumia barabara ya Meli tano- Wete, wamesema zoezi la utiaji wa lami wa barabara hiyo, ndio wameanza kujenga matumiani ya kuitumia barabara hiyo bila ya usumbufu. Walisema, sasa wanaamini na kuanza kusahau machungu waliyodumu nayo kwa miaka zaidi ya 20, kufuatia kuharibika kwa miundombinu ya barabara hiyo bila ya kufanyiwa matengenezo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwa sasa hawana shaka ten ana nia ya serikali ya kuwatengenezea barabara hiyo, hasa baada ya kuanza kwa zoezi la utiaji wa lami wiki tatu zilizopita. Walisema, kwa sasa hawana wasi wasi na kuwataka wenzao wanaoitumia kutoa ushirikiano wa karibu na mafundi hao, ili zoezi hili liwe rahisi kwao. Mmoja katia ya wananchi hao Mwanajuma Haji Nassor ‘anti mwaju’ alisema zaidi ya miaka 30, barabara hiyo ilikuwa ikitajwa kuuanza ujenzi wake bila ya mafanikio. Alieleza kuwa, walifika pahala walishindwa kuamini nia thabiti ya serik...

MIAKA MINNE YA DK. MWINYI: KONDE WAPATA SKULI YA GHOROFA TATU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ameshayatekeleza kwa vitendo, aliyowaaahidi wananchi, ikiwemo ujenzi wa madarasa 2,773 katika skuli zote za Unguja na Pemba. Alisema, Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliitaka serikali kujenga madarasa 1,500 ingawa wameshavuuka lengo hilo, kwa asilimia 184, na bado kazi inaendelea. Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana, mara baada ya kuifungua skuli ya skondari ya ghorofa tatu ya Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za miaka minne ya uongozi wake. Alisema, serikali imepanga hadi kufikia mwaka 2025, iwe imeshajenga vyumba 2,000 vya madarasa katika skuli zote za Unguja na Pemba, ili kuondoa mikondo miwili. Alisema kama kuna watu wanapiga porojo na kusema, uongo waangalie takwimu kutoka wizara ya elimu, zitadhihirisha ahadi zake kwa wananchi. Akizungumza mafanikio mingine, alisema ni kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu...

'JAMBO NIA PEMBA’ : USHIRIKA WA VIJANA WAFUGA NYUKI, WAMILIKI MIZINGA 40, NJIA YA KUKUZA PATO NYEUPE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NI majira ya saa 10: 00 jioni, katika pita pita zangu, niliangukia kijiji cha Fuuweni, kilichomo ndani ya shehia ya Mfikiwa, wilaya ya Chake chake Pemba. Pita pita yangu, ilisikia harufu ya asali kwa mbali, kwa vile mramba asali harambi mara moja, hata hiyo harufu nami sikutosheka kuisikia mara moja. Nilipoangaza macho juu, niliwaona nyuki wakitoka upande wa mashariki na kwenda magharibi mwa kijiji hicho, hapo lakini ghafla niligundua kuwa, ni wale wanaofugwa. Si nilishazoea kila ninapoona nyuki, basi huwa ni wale wa msituni na kufua (kuvuna) unajipangia mwenyewe, lakini kumbe hawa ni wale waliochini ya himaya ya vijana wa kijiji cha Fuuweni shehiani hapo. Sikutaka kuonekana mwizi, la hashaa….nilimvuta kijana mmoja pembeni nikamuuliza, ikiwa wahusika wa wanaofuga mizinga hiyo, wapo karibu ili nizungumze nao. Walishasema wahenga nyota njema huuonekana alfajiri, nami nilibahatika kuzungumza na Msaidizi Katibu wa ushirika huo wa ‘Jambo nia’ Salu...

WAZIRI PEMBE AITANGAAZA KAMPENI YA “MTOTO MBONI YANGU”,

  HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE RIZIKI PEMBE JUMA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUTOA TAARIFA YA KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA “MTOTO MBONI YANGU”, SIKU YA TAREHE 25/10/2024 KATIKA UKUMBI WA WIZARA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO - KINAZINI ZANZIBAR   NDUGU WAANDISHI WA HABARI ASSALAMU ALAYKUM.     Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema ya uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana siku ya leo kwa ajili ya kutoa taarifa ya     KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA MTOTO MBONI YANGU. NDUGU WAANDISHI WA HABARI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto Ajira”   kutoka Dar es Salaam imeandaa kampeni ya kitaifa yenye jina la MTOTO MBONI YANGU , ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Zanzibar.   Lengo kuu la kampeni hii   ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuizunguka nchi nzima ya na kuielimisha, kuiasa na kuzung...