NA MWANDISHI WETU,@@@@ MKURUGENZI muanzilishi kutoka bilali Muslim missin of Tanzania Kairo Nbanu Alidha alisema kuwa, kwa mashirikiano ya Tigozanztel wameamua kuanzisha kambi ya matibabu ya macho siku 3 kisiwani Pemba. Alieleza kuwa tayari wamejipanga katika kuwapatia matibabu wagonjwa 1000 kwa siku, wakiwemo na waupereshi 3000 kwa siku tatu, watakazo kuwepo. Aliyasema hayo huko katika skuli ya Uweleni wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba, wakati alipokuwa akitoa huduma kwa wananchi kutoka sehem mbali. Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kuja kupata huduma hiyo kwa itawasaidia wao na kuhamasisha wenzao ambao, hawakufika kwa siku hiyo. "Huduma ni bure kuanzia dawa, miwani na hata upasuwaji, kwani tunashirikiana na Wizara ya Afya, kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo. Naye katibu wa CCM Neclaus Chibwana, ambaye alifika katika kambi hiyo, kwa kupata matibabu, alieleza kuwa ni vyema kwa shirika hilo, kuendelea kuja kisiwani Pemba, kwajili ya kutoa huduma hiyo,...