Skip to main content

Posts

MTAMBWE KUSINI MAJI 'BWERERE', ZAWA YASEMA JAMBO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mtambwe kusini wilaya ya Wete Pemba, wamesema kwa sasa huduma ya maji safi na salama katika vijij vyao, inapatikana kwa urahisi, tofauti na hapo zamani. Walisema, kwa sasa wamekuwa na wakati mzuri wa kujipangia shughuli zao mbali mbali za kimaisha, na wala upatikanaji wa huduma hiyo, sio changamoto inayowatengulia rataiba zao za kimaisha. Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo, walisema kwa sasa huduma hiyo, iko karibu vijiji vyote, tena bila ya mgao, jambo ambalo limechangia kufikia malengo yao. Walieleza kuwa, upatikanaji wa huduma hiyo kwa miaka minne mfululizo sasa, unawapa uhakika wa maisha yao, hasa kwa vile kila mmoja, anaendesha shughuli zake kwa urahisi. Salma Hamad mkaazi wa kijiji cha Kivumoni, alisema kwa sasa huduma hiyo iko vyema na haina shida kwao, ikilinganisha na miaka 20 iliyopita. ‘’Awali sisi wananchi wa kikijiji cha Kivumoni shehia ya Mtambwe kusini, tukifuata maji masafa ya m...

MKAMA NDUME: MTAWALA MBABE PEMBA KIFO CHAKE KIZUNGUMKUTI HADI LEO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ HAPO zamani Magofu ya Mkama Ndume yalikuwa makaazi ya waswahili, ya enzi za kati, ambayo yaliachwa na wakaazi wake katika karne ya 16.   Ambapo hapo, ilikuwa ni kabla ya Wareno Afrika Mashariki inajulikana kwa uimarishaji wake kwa kutumia mawe. Magofufu hayo yako wastani wa kilomita 10 kutoka katikati ya mji wa Chake chake, ambao ndio makao makuu kwa kisiwa cha Pemba.   Kwa wakati huo mji huo ulitawaliwa na kiongozi mmoja aitwaye Mohammed bin Abdul -Rahman, ambaye alijulikana sana kwa ukatili wake kwa raia wake. Na kwa wakati huo alipewa jina la utani la Mkama Ndume lenye maana ya  mkamua wanaume  kwa lugha ya kiswahili cha zamani. Ndio maana, hadi leo eneo hilo lililojaa historia sio kwa kisiwa cha Pemba pekee, bali baraza zima la Afrika na duniani, pakaitwa Mkama Ndume. Kwa kuwa mtawala alikuwa akifanya ibada, alijenga msikiti wa asili wa Ijumaa, miaka 700 iliyopita, ambao ulikuwa na nguzo...

SKULI YA SEKONDARI CONECTING CONTINENT, ZAO LA MWEKEZAJI LINALOWANYIWA NA WAZALENDO

        NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ SKULI ya sekondari ya Connecting Continent iliyopo nje kidogo ya mji wa Chake chake, ni miongoni mwa skuli 10 binfsi zilizopo kisiwani Pemba. Skuli hiyo ipo nje kidogo ya mji wa Chake Chake, imekuwa ikiwavutia zaidi na wanafunzi wasichana kutokana na upasishaji wake mzuri wa kila mwaka. Conecting ni miongoni mwa skuli 10 binafsi kisiwani Pemba, zilizobahatika kuruhusiwa kuwekeza katika elimu kwa ngazi ya sekondari. Skuli hiyo ilianzishwa mwaka 2006 ikimilikiwa na wawekezaji wajerumani, ikiendeshwa na michango midogo midogo ya wafadhili wenyewe na ada nyepesi zinatolewa na wazazi na walezi.     Skuli hiyo ilianza kufanya mitihani ya taifa mwaka 2008, na kufika mwaka 2022, wanafunzi 671 walihitimu.   Kati ya wanafunzi hao wanawake walikuwa 332 na wanaume walikuwa 339 kwa wakati huo, wakitokea skuli mbali mbali za msingi kisiwani Pemba. Mwandishi wa makala hii hakutaka hadithi za mdomo ali...

MAKOMBENI WAOMBA KUONGEZEWA DOZI ATHARI UTIRIRISHAJI MAJI TAKA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Makombeni wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema bado wanahitaji elimu zaidi ya athari za utiririshaji maji machafu katika makaazi yao, ili kujiepusha na magonjwa ya kuharisha na kutapika. Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika shehiani hapo, walisema bado wapo baadhi yao wamekuwa wakitiririshaji maji hayo, bila ya kujalia afya za wenzao. Walieleza kuw, inawezekana wanaofanya jambo hilo ni kutokujua athari za maji hayo kwa jamii na hasa watoto ambao tahadhari yao ni ndogo. Mmoja kati ya wananchi hao Ali Khamis Juma alisema, moja ya chanzo cha utirirshaji wa maji hayo, ni magonjwa kama ya tumbo la kuharakisha na kutapika. ‘’Ni kweli suala la uchafuzi wa mazingira hasa la utiririshaji maji machafu lipo kwenye shehia yetu, na inawezekana wengi wao hawajui madhara,’’alieleza. Nae Semeni Juma Kheir, alisema hayo yanajitokeza kutokana na kutokuwepo kwa adhabu kali kwa wananchi wanaodharau uchimbaji wa shimo la kuhifadhi maji ...

‘KINJE KUKU’ UTAMADUNI WA MICHEWENI UNAOWAHUSU WATOTO WA KIKE PEKEE

  NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ UTAMADUNI wa uvaaji kanga ya shingoni, ama kwa lugha Micheweni ‘kinje kuku’ umepotea kwa kasi. Kizazi cha sasa cha Micheweni, na hasa watoto wa kike ambao ndio walengwa wa utamaduni, wameanza kuupa kisigo. Wakionekana, kuachana na vazi hilo, na sasa wakivaa nguo nyingine ambazo wanaona zinawastiri hasa sehemu ya kifuani.   Hiyo ni kutokana na karne ya sasa na utandawazi jinsi ulivyokua, ndipo watoto wa kike wa Micheweni takribani kwa asilimia kubwa kuacha utamaduni huo. Vazi hili lilikua linavaliwa sana na watoto, wengi wao wanaishi vijijini, lengo hasa la kinje kuku, ni kuwastiri watoto hao wa kike sehemu ya kifuani, hasa wakianza kutanuka kifua. Vipo vijiji vyengine vingi katika Mkoa huo   ambavyo watoto wa kike walikua wanavaa vazi hilo kama utamaduni wao, lakini mwandishi wa makala hii aliamua kwenda kwenye kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni kuzungumza na wazee.   Wilaya ya Micheweni ni Mkoa unaoongoza kwa masuala ...

WASIOJULIKANA WAIBA MAZAO YA BAHARINI MTAMBWE PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATU wasiojulikana, wamevamia na kuiba Kaa na Vitango bahari, waliyokuwa yakifugwa na wanaushirika wa ‘yashasemwa’ uliopo shehia ya Mtambwe kusini, wilaya ya Wete Pemba. Watu hao kwa nyakati tofauti, wanadaiwa kuiba Kaa 80 kati ya 120 waliyoyaingiza na Vitango bahari kuibiwa yote 1,000 kwa nyakati za usiku.   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, viongozi wa ushirik huo, walisema wizi huo umefanyika miezi mitano, baada ya kuweka vifaranga hivyo, kwa ajili ya ufugaji. Msaidizi wa Mwenyekiti wa ushirika huo Jabir Saleh Jabir, wamepatwa na mshangao mkubwa, baada ya kupokea taarifa za kuibiwa, kwenye shamba lao. Alisema, walitumia gharama kubwa kuanzisha maeneo hayo husika, kwa ajili ya ufugaji wa vitango bahari na Kaa, ingawa watu wasiowafahamu, waliwarejesha nyuma kwa kuwaibia. ‘’Na sisi ni ushirika ambao tuna nia ya kuvuna matunda ya uchumi wa buluu, na tulishajikusanya na kuunganisha nguvu zetu, lakini wengine waliamua kuturejesha ...

MWENGE WA UHURU WATUA PEMBA, WAANZA WILAYA YA WETE UFUNGUZI WA MIRADI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWENGE wa uhuru umewasili kisiwani Pemba, ukitokea Mkoa wa kaskazini Unguja, tayari kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya nne za Pemba, samba mba na ufunguzi wa miradi kadhaa, ikiwemo ya maendeleo kisiwani humo. Mwenge huo umepokelewa jana, katika uwanja wa ndege wa Karume Pemba, ambapo wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, wamejumuika. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahamoud, alisema mwenge huo ukiwa mkoa mwake, ulizindua miradi minane ya maendeleo na program nne, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 14.4. Alisema wakimbiza mwenge, walitoa ujumbe kwa wananchi, ukiwemo suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira, lishe na kupinga rushwa na kisha kuchunguza afya kwa wananchi. Mkuu huyo wa Mkoa, alisema katika kipindi hichi, walipanda miti 120,000, ingawa katika shamra shamra za mwenge wamepanda miti 2,500. ‘’Mkuu wa mkoa wa...

WAZAZI, WALEZI WAWAPA TANO WAALIMU CONNECTING, KAZI IENDELEE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZAZI na walezi wenye watoto wao skuli ya sekondari ya Connecting Continent ya Mgogoni wilaya ya Chake chake, wamesema wameridhishwa na juhudi binafsi za waalimu, katika kuwafundisha wanafunzi skulini hapo. Wakizungumza kwenye mkutano maalum uliofanyika skulini hapo, wenye lengo la kupokea matokeo ya muhula wa kwanza, wazazi na walezi hao, walisema kutokana na ugumu wa wanafunzi ulivyo, wanaridhishwa na juhudi zao. Walisema, wengi wao wamekuwa wakikosa muda wa kuwauliza watoto wao juu ya maendeleo ya elimu, lakini waalimu hao, wamekuwa wakibuni mbinu za kuwaendeleza wanafunzi. Wazazi hao walieleza kuwa, kwa muhula huu kwanza, wameridhishwa na matokeo hayo, ambayo kwa yale ya darasa la 12, kama yengekuwa ndio ya mitihani ya taifa, kusingekuwa na mwanafunzi aliyefeli. Mmoja kati ya wazazi hao Omar Mjaka Ali, alisema kama sio juhudi za waalimu hao na mbinu mbali mbali za kuwalazimisha wanafunzi kusoma, matokeo ya muhula wa kwanza, yasingekuwa maz...