NA HAJI NASSOR, PEMBA MOJA ya sheria kongwe na inayotajwa kutokwenda sambamba na uhuru wa vyombo vya habari, ni ile nambari 5 ya mwaka 1988 ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari Zanzibar. Ni miaka 34 sasa, sheria hii inaendelea kutumika Zanzibar, na kutajwa kuathiri na kutishia utendaji kazi wawaandishi wa habari visiwani. HISTORIA Sheria hiyo tokea mwaka 2010, ilianza harakati za kutaka kufutwa, kwa wadau wa habari kujikusanya pamoja, ili sasa iwe na sheria moya ya habari. Kwa wakati huo, tasisi za Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ –ofisi ya Zanzibar, vyama vya waandishi wa habari, taasisi za haki za binadamu na wizara husika, zilianza harakati hizo. Mara kadhaa, kulikuwa na taarifa kuwa, mwaka ujao au mwakani Zanzibar itapatikana sheria mpya ya habari, ambayo itakuja kufuta sheria ya Magazeti nambari 5 ya mwaka 1988 na ile ya Tume ya Utangaazji nambari 7 ya mwaka 1977. Ilikuchakua takriban miongo miwili, kupita bila Zanzibar kuwa na sheria mpya, ingawa kwa Tan...