NA HAJI NASSOR, PEMBA
MOJA ya sheria kongwe na inayotajwa
kutokwenda sambamba na uhuru wa vyombo vya habari, ni ile nambari 5 ya mwaka
1988 ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari Zanzibar.
Ni miaka 34
sasa, sheria hii inaendelea kutumika Zanzibar, na kutajwa kuathiri na kutishia
utendaji kazi wawaandishi wa habari visiwani.
HISTORIA
Sheria hiyo
tokea mwaka 2010, ilianza harakati za kutaka kufutwa, kwa wadau wa habari
kujikusanya pamoja, ili sasa iwe na sheria moya ya habari.
Kwa wakati
huo, tasisi za Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ –ofisi ya Zanzibar, vyama vya
waandishi wa habari, taasisi za haki za binadamu na wizara husika, zilianza
harakati hizo.
Mara kadhaa,
kulikuwa na taarifa kuwa, mwaka ujao au mwakani Zanzibar itapatikana sheria
mpya ya habari, ambayo itakuja kufuta sheria ya Magazeti nambari 5 ya mwaka
1988 na ile ya Tume ya Utangaazji nambari 7 ya mwaka 1977.
Ilikuchakua
takriban miongo miwili, kupita bila Zanzibar kuwa na sheria mpya, ingawa kwa
Tanzania bara, wao walifanikiwa kufuta sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, na
kuwa na sheria ya Huduma ya vyombo vya habari ‘MSA’ ya mwaka 2016.
Aliyewaji
kuwa Katibu mkuu wizara ya Habari Ali Mwinyikai, alisema iko siku Zanzibar, itakuwa
na sheria bora na iliyorafiki kwa waandishi wa habari.
Hata aliyekuwa
Mhariri Mtendaji wa shirika la Magazeti ya serikali Zanziba Abdalla Mohamed
Juma, aliwahi kusema, sheria ya magazeti, iliyopo sasa, haiendani na upevukaji
demokrasia.
Kwa miongo
miwili, wadau wa habari juhudi zao za kuwa na sheria mpya ya habari ziligonga
ukuta, na harakati hizo zikaanza tena miaka ya 2018/2019.
YANAYOWASKUMA WADAU KUFUTWA KWA SHERIA
YA MAGAZETI, VITABU NA MAWAKALA WA HABARI NO 5, 1988.
Sheria hii
yenye vifungu 81 na sehem 10, sasa inatimiza miaka 34, tokea kutungwa kwake, na
kwa maana nyingine, vipo vifungu zaidi ya 40, ambavyo vyengine vinahitaji
kufutwa.
Vifungu
vyengine vikihitajika kufanyiwa marekebisho na vyengine, vilivyobeba maneno
makali kama uwezo wa waziri, waandishi kudhibitiwa na kufanya uchochezi.
Kwenye
sheria hii, ambayo kwa sasa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania
TAMWA-Zanzibar kwa ufadhili wa Internews, wanaharakishwa kufutwa kwa sheria
hiyo.
VIFUNGU KANDAMIZI KWA UHURU WA HABARI
Moja ya
kifungu ambacho, kwa sasa wadau wanataka kifutwe ni kile cha 43, ambacho
chenyewe, kinaeleza ‘uwezo wa ofisa aliyeidhinishwa’.
Ambapo kwa
mujibu wa sheria hiyo, ofisa aliyeidhinishwa ni Polisi mwenye cheo cha Msaidizi
Ofisa Mkaguzi au mwenye cheo cha juu ya hapo.
Mchambuzi wa
sheria za habari Zanzibar Hawra Shamte anasema, kwa sasa sheria hiyo na hasa
kifungu cha 43 wanakiona, hakina mantiki.
‘’Makosa
yote yanayotokana na waandishi wa habari yana sura ya madai na sio jinai, sasa
iko wapi nafasi ya Polisi kuingia, kupekua kwenye vyombo vya habari,’’anahoji.
Ukali wa
mchambuzi huyu wa habari, unajidhihirisha kwenye kifungu hicho cha 43 (1) na (2)
ambavyo vimeeleza wazi mamlaka ya ofisi huyo wa Polisi.
‘’Mfano
kifungu (2) (a) kinaeleza uwezo wa ofisi huyo kuwa ‘anaweza kuingia sehemu yoyote, jengo,
chombo cha ardhini, angani ambamo anaamini kwa maoni kuwa, mna vifaa vya
habari, vilivyopangwa au vitakavyopangwa kukusanyia habari,’’
Hata kifungu kidogo cha 2 (b) kikaongeza kuwa,
ofisi huyo anaweza ‘kuchunguza mchakato wowote ambao unaonekana kuelekea kukusanya au
kutoa habari yoyote ’.
Kubwa zaidi
ambalo ni ukiukwaji wa uhuru wa habari, kifungu cha (c) kinampa uwezo ofisi
hiyo ‘kumtaka mwandishi wa habari yeyote, kutoa vitendea kazi vyake, gazeti
au waraka ambao, uko chini yake kukabdhi kwake’.
Kifungu 2 (d)
ofisi huyo amepewa mamlaka ya ‘kunakili sehemu yoyote ya vitendea kazi
vya waandishi wa habari au akiamiani tu kufanya hivyo, kuna uhusiano na
uchunguuzi wake juu ya kosa chini ya sheria hii’.
Kubwa zaidi,
pia ofisi hiyo kwenye kifungu hicho cha 43 (2) (e) anaweza ‘kuagiza
taarifa zenye uhusiano na uchunguuzi wake kutoka kwa mtu yeyote, ambae anaamini
aliajiriwa au ataajiriwa katika jengo alilokuwa akitunza kumbu kumbu’.
Pamoja na
uwezo huo, ambao wadau wa haki za uhuru wa habari wanaona ni uminywaji wa haki
za waandishi wa habari, sasa kifungu cha 44 kimekuja kumlinda.
Kifungu
hicho 44 (1) kinaeleza kuwa, ‘mtu yeyote atakayempinga, kumzuia, au
kumkwaza kwa ofisa huyo atakuwa ametenda kosa’
Na adhabu
kwa kosa hilo lipo kifungu cha 73, ambapo ni faini ya shilingi 200,000 au
kifungo cha miaka miwili chuo cha mafunzo au adhabu zote mbili kwa pamoja.
WADAU WA HABARI WANASEMA JE?
Meneja wa
redio Jamii Micheweni Ali Massoud Kombo, anasema kifungu hicho sio rafiki, na
hakitarajii kukiona kwenye sheria mpya ijayo ya habari.
Anasema,
studio na vyumba vya habari ni ofisi nyeti kama zilivyonyengine, hivyo utaratibu
wa kuingia, uwepo kama zilivyo ofisi nyingine.
‘’Mbona
Ikulu, wodi ya wazazi, kambi za Jeshi na hata chuo cha mafunzo kuna utaratibu
wake, na sio ofisa yeyote tu Polisi tena kwa maoni yake aweze kuingia,’’anahoji.
Mmiliki wa
mawio tv online Suleiman Rashid Omar, anasema kifungu hicho hakifai kuwepo,
maana kinahalalisha ukandamizaji wa uhuru wa waandishi wa habari.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ Kajubi Mukajanga wakati akizungumza
na waandishi wa habari kisiwani Pemba wiki iliyopita, alisisitiza vyombo vya
dola kuwaachia waandishi watekeleze kazi zao.
‘’Kuwapasha
habari wananchi juu ya matukio ya ndani na nje ni haki kikatiba, sasa kama kuna
sheria au kifungu kinampa uwezo mkubwa Polisi kuingia na kufanya atakavyo sio
sahihi,’’anasema.
Mratibu wa
TAMWA -Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema uhuru wa waandishi
wa habari ni mbolea kwa taifa kutimiza malengo yake.
‘’Lakini
sheria yetu ya Mgazeti nambari 5 ya mwaka 1988 ya Zanziba na hasa kifungu cha
43 kinaipinga hata katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, iliyotoa haki ya kutoa
maoni,’’anaeleza.
Mjumbe wa
Kamati tendaji wa Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAZA’ Hidaya
Mjaka Ali, anasema sheria bora ni chachu ya kupata waandishi wa habari bora.
Mkurugenzi
wa vijana Pemba Ali Mussa anasema wanawategemea mno waandishi wa habari
kuwaibulia changamoto za vijana na kuwaonesha njia.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa kuskazini Pemba Juma Saadi Khamis anasema, sio maoneo kama
vyumba vya habari kuwa ofisa, anaweza kuvamia ikiwa hakuna uhalifu.
Mdhamini wa
Baraza la Habari Tanzania MCT-Zanzibar Shifaa Said Hassan, anasema sheria hiyo
imeshapitwa na wakati na moja ya vifungu vibaya ni cha 43 na vifungu vyake
vidogo.
‘’Haiwezekani
suala la haki ya kikatiba ya kupata na kutoa habari, apewe uwezo wa kupindukia Polisi,
juu ya kuingia na kupekua kwenye ofisi za waandishi wa habari,’’anasema.
Mchambuzi wa
sheria za Habari Zanzibar Hawra Shamte anasema, kwenye nchi zinazojali kwa
vitendo utawala bora na utawala wa sheria, suala la kupata na kutoa habari
haliwekewi masharti mazito.
Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari na
Mawasiliano ya Umma Zanzibar Imane Duwe, anasema dunia ikisherehekea ukuaji wa teknologia
kwenye eneo la habari, lazima waandishi wawe huru.
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari Zanzibar ‘ZPC’ Abdalla Abudull-rahman Mfaume na
mwenzake wa PPC Bakari Mussa Juma, wanasema vifungu ambavyo vinampa wasi wasi
waandishi wa habari havina nafasi Zanzibar.
Mhariri wa
habari wa shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar Juma Khamis Juma aliwahi
kusema kuwa, ukuaji wa maendeleo ya taifa lolote duniani, waandishi wa habari
mchango wao upo.
NINI KIFANYIKE?
Kaimu
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ Pemba Safia Saleh Sultan,
anasema lazima kwenye sheria ijayo ya habari, kifungu hicho kifutwe.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wasioona ‘ZANAB ‘Pemba Suleiman Mansour, amesema lazima suala la
vyumba vya habari au wao wenyewe kupekuliwa lisiwe la kila ofisa wa Polisi.
‘’Sheria
ijayo ya habari, sitamani kurejeshwa kwa kifungu hichi, maana kwa upande
mwengine ni kudhoofisha juhudi za waandishi katika kazi zao,’’anasema.
Afisa
Mdhamini wizara ya Habari Pemba Mfamau Lali Mfamau, anasema ukandamizwaji wa
waandishi wa habari, hudhoofisha maendeleo ya taifa.
Mkuu wa
wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, anasema sheria bora ya habari huchangia
kuwa na jamii bora na inayofanya uamuzi sahihi.
Mwandishi wa
habari wa kituo cha tv na redio cha Zenj fm Amina Ahmed, anasema sheria hiyo
hasa kwenye upatikanaji wa kibali umekuwa shida.
Mkurugenzi
wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzur Issa Ali, anasema ujio wa sheria mpya ya habari vifungu
vinavyompa uwezo mkubwa waziri visiwmo.
Mratibu wa uchechemuzi
wa upatikanaji wa sheria ya habari Zanzibar kutoka TAMWA-Zanzibar Muhammed
Khamis, anasema wakati umefika Zanzibar kuwa na sheria rafiki.
‘’Ndio maana
TAMWA -Zanzibar kwa kushirikiana na wafadhili wetu Shirika la Internews
Tanzania tunaomradi wa miezi minne, ili kuwawezesha waandishi, kusukuma
upatikanaji wa sheria mpya habari Zanzibar,’’anasema.
Mwisho
Comments
Post a Comment