NA HAJI NASSOR, PEMBA KUTOKUWA na migogoro nchini ni sababu kubwa inayopelekea kuendelea kwa shughuli za kimaendeleo na kufikia jamii yenye amani. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa mradi wa ‘Jenga Amani Yetu’,Khamis Haroun Hamad alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya nafasi ya wanasiasa kujenga amani ya Zanzibar. Alisema, ili jamii iweze kuwa na amani na kufikia maendeleo endelevu, kunahitaji ushirikiano wa pamoja katika kutatuwa migogoro inayoikabili jamii, huku wanasiasa wakiwa na nafasi kubwa . Alifahamisha kuwa, suala la kutatua migogoro si la mtu mmoja pekee, bali ni la watu wote, hivyo ni vyema kila mmoja kuchukuwa nafasi yake katika jamii ili lengo liweze kufikiwa. “Sisi hatuwezi kutosha lakini tukichanganyika na nyinyi mukapeleka kwa wengine, mafanikio yatapatikana kwa haraka”,alisema. Alieleza kuwa lengo la mradi huo ni kuifikia jamii na kuisambaza elimu hiyo, ili kila mmoja ahakikishe analinda haki yake ...