Na Haji Nassor, PEMBA
“Moto ni mtu aliechini ya miaka 18’’ ndivyo
sheria namba 6 ya mtoto ya mwaka 2011 ya Zanzibar inavyotoa tafsiri ya nani mtoto.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yenyewe
imeridhia kuwa mtu hatoweza kupiga kuram kama iwapo hatotimizia masharti
yaliopo likiwemo la kufikia umri wa miaka 18.
Nayo katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, imekwenda mbali zaidi kwamba mtu hatochaguliwa kuwa
rais kama hajatimiza umri wa miaka 40.
Huku taifa la Tanzania likifatua katiba
mpya, hata rasimu ya awali ya katiba hiyo iliotolewa Juni 3 mwaka 2013, pamoja
na mambo mengine, imerudi ikitaja umri wa miaka 18 ndio wa mtu uzima ndani
taifa hili.
Tafsiri hii, imekuwa ikiiumisha kichwa
jamii ya Zanzibar ambayo asilimia 99, imekuwa ikifuata Imani ya dini ya
kiislamu na kuwepo kwa tofauti kubwa.
Ingawa tasfsiri ya nani mtoto huja kutokana
na mazingira yake, na ndio maana kumbu kumbu zinaonyesha kuwa hata wakati wa
ukoloni baadhi ya sheria hazikutaja umri wa miaka 18 kama ndio mtu mzima, bali
ni mbali zaidi.
Sheria namba 6 ya elimu Zanzibar ya mwaka
1982, kifungu cha 19 kimetamka kuwa ‘itakuwa ni lazima kwa kila mtoto aliefikia
umri wa miaka saba (7) lakini hajafikia umri wa miaka 13, kuandikishwa elimu ya
msingi, na kifungu kidogo cha (3) kuwa, haruhusiwi mwanafunzi kuoa au kuolewa
kabla ya kumaliza elimu ya msingi au sekondari ya awali.
Kumbukumbu hizo zilionyesha kuwa, sheria ya
watoto na vijana ya ‘cap’ 58 ya mwaka 1952, sheria hii ilikaribiana na kabisa
na imani za waumini wa dini ya kiislamu, maana yenyewe ilimtambua mtoto ni yule
aliechini ya miaka 14 na sio miaka 18.
Ingawa sheria hii ilifutwa na sheria na
kanuni mbali ikiwemo, sheria namba 6 ya mwaka 2011 ambayo yenye ilimtambua
mtoto ni yule aliechini ya umri wa miaka 18, jambo ambalo jamii ya Zanzibar
inakinzana na sheria hii.
Sheikh Mohamed Adamu Makame kadhi wa wilaya
ya Mkoani, alisema inaweza kuwawiya vigumu wananchi wa Zanzibar, kuona kama ni
kosa kumuozesha mtoto aliechini ya miaka 18, kwa vile Imani zao hilo
haliendani.
‘’Wazanzibar ambao wengi wao wanafuata
Imani ya dini ya kiislamu, wanaamini kuwa mtoto kwao ni yule ambae hajabaleghe
kwa mwanamme na wa kike ambae hajapata ukubwa, na sio vyenginevyo’’,alisema.
Nae sheikh Mohamed Said wa mji wa
Chakechake, alidakiza kuwa kuwa, ni vigumu kuwakataza wazazi ambae mwanae
ameshamaliza masomo na amepata mume akiwa na miaka 17, eti kumsubiria mapaka
atimize miaka 18.
‘’Kama seikali inataka kutokomeza ndoa na
mimba za utotoni, lazima sheria zetu zimwe na mahusiano na Imani za wananchi
wake waliowengi, kama ilivyokuwa na sheria za Sultan za kumtambua mtoto akiwa
chini ya maika 14’’,alishauri.
Mzazi Hassan Rajabu Jecha (54) wa shehia ya
Tibirinzi, yeye haoni kwamba ni kosa kumpa mwanae wa kike mume, eti kwamba
hajatimiza miaka 18, kama inavyotaka sheria.
Mzazi Bikombo Simai Juma (45) wa shehia
Kichungwani wilaya ya Chakechake, kwa upande wake, aliishauri serikali na
watungaji sera hasa ambazo zinaonekana na maslahi kwa mtoto, kuhakikisha
hazipingani sana na Imani zao.
‘’Mimi wanangu watatu wote niliwaozesha
chini ya miaka 18, maana mmoja hakutaka kwenda skuli, mwengine alinijia na
ujauzito na mwengine alifeli darasa la kumi, lakini kidini hawa sio watoto
tena’’,alifafanua
Hakimu wa Mahakama ya mkoa Chakechake
Khamis Ramadhan Abdalla, alikiri kukumbana na changamoto kama hizo kwenye kesi
za mimba kutokana na jamii kufuata zaidi Imani zao za dini.
‘’Chakufanya ili kuondoa mimba na ndoa za
utotoni, ni kwa wahusika wa utungaji wa sheria, kuhakikisha kuna uwiyano baina
ya sheria hizo na imani za walengwa wa sheria’’,alifafanua.
Mgongano huo wa tafsiri wa nani mtoto
ulioanzia hata kabla ya taifa la Tanzania na Zanzibar kujitawala miaka ya 1963
na 1964, sio gumzo wala tatizo kwa waumini wa dini ya kiislamu eti kuoa au
kuolewa mtoto aliechini ya miaka 18.
Lakini hata wataalamu wa magonjwa ya akina
mama hawakubaliani na umri wa miaka 18, kwamba ndio mtu mzima na tayari kwa
kubeba ujauzito.
‘’Sisi hushauri sana kwamba umri sahihi wa
kubeba ujauzito ni kuanzia miaka 20 maana hapo ndio viungo na mwili wake
umeshajitayarisha kwa kuhidhi kiumbe’’,alisema dk Namie Ali.
Umri wa miaka 18 sio ruhusa ya kufanya kila
jambo, inawezekana ni kwa ajili ya mambo mengine ya kiserikali na shughuli za
kijamii.
Wanaharakati mbali mbali wa kupinga mimba
na ndoa za utotoni, kwamwe haiingilii Imani za kundi moja au jengine, huku
kubwa zaidi wakisistiza elimu kwa mtoto wa kike.
“Lakini kwa nini jamii hiyo inayofuata
Imani za dini ya kiislamu, ikimbilie zaidi kwenye sunna ya ndoa na kuacha
faradhi ya elimu kwa watoto wao’’,alitamka Mratibu wa Chama cha waandishi wa
habari Wananwake Tanzania TAMWA afisi ya Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali.
Wasatini wa kesi 20 hadi 25 za mimba na
ndoa za utotoni kwa mwaka mmoja, zimekuwa zikifuatiliwa kwa kina na TAMWA, na
hasa hupata ushirikiano baada ya kuwapa taaluma familia na watoto wa kike.
Jamii
haina budi kuweka mkazo maalum wa kuwasomesha watoto wao wa kike, ili waweze
kujikomboa na kufahamu haki zao na kuondokana na utegemezi katika familia zao.
Fatma Marzouk Kombo yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia kuelimisha Athari
za madawa wa kulevya, ukimwi na mimba za utotoni ‘JUKAMKUM’ , alisema tokea
walipoanzisha jumuia yao, wamekaa kwa muda wa zaidi ya miaka mitano bila ya
kupata fedha za kufanya kazi zao.
‘’Sisi tunakusudia kuwafikia watoto wa kike
zaidi ya 2,000 kuwapa elimu ya kujikinga na mimba na ndoa za utotoni na
tuliomba mradi kwa asasi kubwa ya kiraia na tumefanikiwa’’,alisema.
Hapa aliiomba jamii kuhakikisha wanawaunga
mkono, ili kutokomeza wimbi la watoto wa kike kupata ujauzito na wakiwa chini
ya umri wa miaka 18.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa kusini Pemba,
wametaja chanzo cha mimba na ndoa z autotoni kuwa ni pamoja na mporomoko wa
maadili ambao umechangiwa na utandawazi.
Muathirika wa ndoa ya utotoni mwenye (16)
mkaazi wa shehia ya Kichungwani Chakechake, alisema yeye alilazimishwa kuacha
masomo na wazazi wake, baada ya kutokezea waume wawili mfululizo.
“Alikuja mume wa kwanza niko darasa la
tisa, na wa pili alikuja naanza kuingia darasa la kumi mwaka 2011 skuli ya
Madungu na babaka akasema niloewe, na sasa nimeshaachwa’’,alifafanua.
Kijana huyo ambae kwa sasa yuko kwao shehia
ya Kichungwani, aliolewa Juni mwaka 2012 na mwezi Mei mwaka 2013 aliachwa, na kwa
sasa anatamani kurejea masomoni.
Baba wa kijana huyo miaka (55) alisema hilo
lilijitokeza baada ya kutalikiana na mke wake, na mtoto huyo alikuwa akilelewa
na bibi yake na baada ya kuonekana amebadili tabia ndio alifikia uamuzi huo.
Nae sheikh Ahmad Said kutoka afisi ya Mufti
Pemba, alisema suala hilo linahitaji nguvu ya pamoja, ili kutokomeza mimba kwa
watoto.
Mchungaji Benjamin Kissanga wa kanisa katoliki
la kilutheri Tanzania, liliopo Alikhamis Chakechake, alisema maandiko
yanakataza kuwakatisha masomo watoto, kwa kuwaozesha waume.
Idadi ya kesi za mimba na ndoa za utotoni
zinaokena kutisha ndani ya mkoa wa kusini Pemba, na ndio maana kitakwimu ndani
ya miaka miwili iliyopita wanafunzi wenye uwezo kujaa madarasa matatu 196
walikumbwa na majanga ya kuolewa na kupewa ujauzito.
Uchunguuzi ukabaini kuwa katia hao, 122
wameripotiwa kupewa ujauzito na 74 kuolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18,
kuanzia kipindi cha mwezi Januari mwaka 2021, hadi mwezi novemba mwaka huu mkoa
wa kusini Pemba.
Mwaka mmoja pekee, kesi za mimba za utotoni zilikuwa 73,
wakati kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba mwaka 2013, ziliripotiwa kesi 49
za mimba kwa wanafunzi.
Kesi za ndoa kwa wanafunzi, kulikuwa na
idadi ya 54, kwa mwaka 2020 na mwaka 2021 kulipripotiwa kesi 20 katika taasisi
mbali mbali.
Wizara ya elimu pekee ilikusanya jumla ya
kesi 67 za mimba na ndoa, ambapo kati ya hizo, mwaka 2012 kesi za ndoa zilikuwa
38, wakati kesi za mimba kwa wanafunzi zilikuwa 14, wakati mwaka huu
kumesharipotiwa kesi 9 za ndoa na 6 za mimba.
Shehia za Tibirinzi, Kichungwani na Madungu
wilaya ya Chakechake kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 zilirpoti kesi 25 za mimba
na ndoa za utotoni, ambazo zote uchunguuzi umegundua zilifikishwa kituo cha
Polisi wilayani humo.
Vyanzo mbali mbali vya habari, vilisema chanzo
cha kujitokeza kwa matendo hayo husababishwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja
na uhuru mkubwa wa wazazi wanaowapa watoto wao wa kike.
Sheha wa shehia ya Madungu wilaya ya
Chakechake, Mafunda Hamad Rubea, aliweka wazi kuwa, kwa karne hii wazazi
wamejisahau na kuwapa uhuru mkubwa watoto.
“Idadi ya kesi za mimba za utotoni zinaweza
kuendelea kukuka siku hadi siku, kama wazazi wataendelea kuwaogopa watoto wao
na kuwapa kila watakacho’’,alifafanua.
Afisa Mkuu wa dawati la jinsi na watoto la
Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, Asha Talib alisema kesi za mimba na ndoa
za utotoni, zimekuwa tatizo sugu, kutokana na watendaji, na waathirika kuwa
ndugu wa familia.
“Hata sisi dawati wakati mwengine hupata
ugumu mkubwa wa kuzishughulikia kesi hizi, maana utakuta aliempa ujauzito mtoto
ni kaka, ami, baba wa kambu, au mwalimu wake, sasa wanakua wazito hata kutoa
ushahidi”,alifafanua.
Mratibu wa kituo cha mkono kwa mkono,
Chakechake Fatma Abdalla Ali alisema, chanzo cha kesi hizo, ni kutokana na
Polisi kuzifanyia sulhu kesi hizo katika hatua za awali.
‘’Polisi wamekuwa kama wanazichechea kesi
za ndoa na mimba za utotoni, maana wamekuwa wakijifanya mahakama kwa kutoa
sulhu, wakati walipaswa wazipekeleke juu’’,alifafanua.
Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 dawati
la jinsia na watoto la mkoa wa kusini Pemba,
liliripoti kesi 13, wakati kituo cha mkono kwa mkono kiliripoti kesi 61,
huku wizara ya uwezeshaji ustawi wa jamii maendeleo ya wanawake na watoto,
ilipokea kesi zaidi ya 30.
Wakati hayo yakijiri utafiti uliofanywa shirika
la Plan la Uengereza limebaini kuwa watoto 14 milioni kwa mwaka waliochini ya
umri wa miaka 18 huingia katika ndoa za mapema.
Huku nchi za Nigeria ikiwa na asilimia 75,
ikiwafuatiwa na Chad yenye asilimia 68 sawa na Afrika ya kati, ambapo nchi ya Bangladeshi
ikiripotiwa kua na asilimia 66 ya watoto wanaoolewa wakiwa chini ya umri wa
miaka 18 nchi nyengine ni Mali, Georgia, India, Turkey na Ukraine zikitaja na
utafiti kua ndio zinazoongoza.
Ambapo pia asilimia 48 ya wanawake wote
walioolewa Uguja mkoa wa Kaskazini, waliingia kwenye ndoa wakiwa na umri kati
ya 12 hadi 18, ikitofauti na wale wenzao wa kisiwa cha Pemba ambao pia utafiti
huo ulioangaza na ukabaini kuwa, wanawake wenye umri wa miaka 12 hadi 18 sawa
na asilimia 62, yaani kila wanawake 100 wanaoloewa 62 hua na umri huo.
Hata
hivyo ndani mwaka huu, tayari mahakama ya mkoa wa Chakechake, imeshawahukumu
washitakiwa wanne akiwemo Abuu-bakari Mkulu Bakari (28), aliefungwa miaka 60
jela kwa kuwabaka watoto wawili, na Ali Mohamed Ali (22) alietiwa kifungoni
miaka 30 nae kwa kosa la ubakaji.
Wakati umefika kwa jamii kufanga kibwebwe
na kuona kua suala la mimba na ndoa za utotoni haziwatendei haki watoto wa
kike.
Mwisho
Comments
Post a Comment