NA HAJI
NASSOR, PEMBA
WANANCHI kisiwani
Pemba, wametakiwa kuendelea kuchukua hatua za kuchunguuza afya zao mara kwa
mara, ili wajielewa ikiwa wanaishi na vimelea ambavyo vinaweza kusababisha
ugonjwa wa kifua kikuu ‘TB’.
Ushauri huo umetolewa na mtaalamu kutoka kitengo shirikishi cha maradhi ya ukoma, kifua
kikuu na Ukimwi Zanzibar, Said Khamis Ahmada, wakati akizungumza na mwandishi
wa habari hizi.
Alisema, moja
ya njia ya kujikinga ama kuwahi matibabu ya ugonjwa huo, ni kuwa na tabia ya
kuchunguuza afya mara kwa mara, ii upatikane ufumbuzi kwa wataalamu wa afya.
Alieleza
kuwa ugonjwa wa kifua kikuu kitaalamu unaoitwa (‘Tuberculosis’ TB) ni miongoni mwa magonjwa 10
yanayosababisha vifo kwa wingi duniani kote.
Alifahamisha
kuwa tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni ‘WHO’ zinaonesha kuwa, inakisiwa
watu milioni 10 wameugua ugonjwa huo, duniani kote, na hadi mwaka 2020, na kati
ya hao watu milioni 1.5 wamefariki dunia.
‘’Utafifi
huo ukagundua kuwa, kwa Zanzibar inakisiwa kuna wagonjwa 124 katika kila watu 100,000 ambapo hii ni
sawa na wagonjwa 1, 612 kwa mwaka, hivyo nasi hatuko salama,’’alifafanua.
Katika
hatua nyingine mtaalamu huyo, alibainisha kuwa, hadi mwaka 2021, Zanzibar
kuligundulika wagonjwa 1, 090 ambapo hao ni sawa na asilimia 68, na vifo
vilikuwa swa na asilimia sita katika mwaka 2020.
Kwa upande wake Mratibu wa
Kikfua kikuu na Ukoma kanda wa Pemba Dk. Hamad Omar Hamad, alisema moja ya
dalili za za ugonjwa huo ni kikohozi cha muda mrefu kuanzia wiki 2 au zaidi.
Alieleza kuwa, dalili nyingine ni kukohoa makohozi ambayo
wakati mwengine huchanganyika na damu, ambayo huanza mapesi mepesi mfano wa
mafuta ya nazi na kisha kuwa mazito mfano wa mafua mapevu.
‘’Hata kutokwa na jasho jingi wakati wote na hasa
nyakati za usiku, hata kama hali ya hewa ni ya baridi, ambapo mtu huyo
hushauriwa kufanya vipimo,’’alisisitiza.
Nae mtaalamu wa
magonjwa ya kifua kikuu na ukoma kutoka kitengo shirikishi Zanzibar Valeria
Rashid, anasema matibabu ya ‘TB’ huchukua kati ya miezi sita (6) hadi mwaka mmoja.
Ambapo anasema mgonjwa
anatakiwa kula dawa chini ya usimamizi (nyumbani au kituo cha afya)
kilichokaribu naye, ili kupata uhakika wa dozi vizuri.
Akizugumza hivi karibuni, ‘Waziri
wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui anasema vituo vyote vya afya vya watu
binafsi na serikali, vinatoa matibabu bila ya malipo, kwa wagonjwa wa TB.
‘’Ni fursa kwa wananchi kufanya
uchunguuzi wa afya zao, na ikiwa wamegundulika na TB wanapewa matibabu bure
katika vituo na hospitali zote za serikali na watu binafsi,’’anaeleza.
Meneja Mpango wa
Shirikishi wa magonjwa ya Ukimwi, Kifua kikuu na Ukoma Pemba Khamis Hamad
Khamis, alisema vyombo vya habari ni nyenzo pana ya kutoa elimu ya kupambana na
magonjwa hayo.
mwisho
Comments
Post a Comment