Skip to main content

Posts

WEMA: YATOA TAHADHARI WANAOSUBIRI AJIRA ZA UALIMU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imewatahadharisha wazazi, walezi na vijana wanaosubiri ajira za uwalimu, kuwa makini kwani, kwani matapeli wanaweza kuingilia kati zoezi hilo. Wizara hiyo imesema, matapeli wanaweza kuwahadaa wazazi, walezi au wataka ajaira hizo, na kuanza kuwapa maelekezo mingine yasiokuwa au yanayofafana na ya wizara, ili kuwatoleshea fedha. Akizungumza na waandishi wa habari Pemba, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said, alisema ni kweli, katika mwaka huu wa fedha, wizra inaompango wa kuajiri waalimu, lakini nao matapeli wanaweza kutumia fursa hiyo. Alieleza kuwa, ndio maana wizara imeona iwatahadharishe wazazi na vijana wenyewe mapema, ili zoezi litakapoanza lisije kuwaathiri wananchi. Katibu mkuu huyo alieleza kuwa, maana wakati huo wa zoezi likiwa katika mchakato, wapo wanaoonekana kulalamikiwa, baada ya kupigiwa simu wakiahidiwa kusaidiwa kupata ajira hizo. ‘’Wizara ya Elim una Mafunzo ya Amali, i...

HATIMAE BARABARA MELI TANO- WETE YAANZA KUTIWA LAMI, WANANCHI HAWAAMINI MACHO YAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI na waendesha vyombo vya moto wanaotumia barabara ya Meli tano- Wete, wamesema zoezi la utiaji wa lami wa barabara hiyo, ndio wameanza kujenga matumiani ya kuitumia barabara hiyo bila ya usumbufu. Walisema, sasa wanaamini na kuanza kusahau machungu waliyodumu nayo kwa miaka zaidi ya 20, kufuatia kuharibika kwa miundombinu ya barabara hiyo bila ya kufanyiwa matengenezo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwa sasa hawana shaka ten ana nia ya serikali ya kuwatengenezea barabara hiyo, hasa baada ya kuanza kwa zoezi la utiaji wa lami wiki tatu zilizopita. Walisema, kwa sasa hawana wasi wasi na kuwataka wenzao wanaoitumia kutoa ushirikiano wa karibu na mafundi hao, ili zoezi hili liwe rahisi kwao. Mmoja katia ya wananchi hao Mwanajuma Haji Nassor ‘anti mwaju’ alisema zaidi ya miaka 30, barabara hiyo ilikuwa ikitajwa kuuanza ujenzi wake bila ya mafanikio. Alieleza kuwa, walifika pahala walishindwa kuamini nia thabiti ya serik...

MIAKA MINNE YA DK. MWINYI: KONDE WAPATA SKULI YA GHOROFA TATU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ameshayatekeleza kwa vitendo, aliyowaaahidi wananchi, ikiwemo ujenzi wa madarasa 2,773 katika skuli zote za Unguja na Pemba. Alisema, Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliitaka serikali kujenga madarasa 1,500 ingawa wameshavuuka lengo hilo, kwa asilimia 184, na bado kazi inaendelea. Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana, mara baada ya kuifungua skuli ya skondari ya ghorofa tatu ya Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za miaka minne ya uongozi wake. Alisema, serikali imepanga hadi kufikia mwaka 2025, iwe imeshajenga vyumba 2,000 vya madarasa katika skuli zote za Unguja na Pemba, ili kuondoa mikondo miwili. Alisema kama kuna watu wanapiga porojo na kusema, uongo waangalie takwimu kutoka wizara ya elimu, zitadhihirisha ahadi zake kwa wananchi. Akizungumza mafanikio mingine, alisema ni kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu...

'JAMBO NIA PEMBA’ : USHIRIKA WA VIJANA WAFUGA NYUKI, WAMILIKI MIZINGA 40, NJIA YA KUKUZA PATO NYEUPE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NI majira ya saa 10: 00 jioni, katika pita pita zangu, niliangukia kijiji cha Fuuweni, kilichomo ndani ya shehia ya Mfikiwa, wilaya ya Chake chake Pemba. Pita pita yangu, ilisikia harufu ya asali kwa mbali, kwa vile mramba asali harambi mara moja, hata hiyo harufu nami sikutosheka kuisikia mara moja. Nilipoangaza macho juu, niliwaona nyuki wakitoka upande wa mashariki na kwenda magharibi mwa kijiji hicho, hapo lakini ghafla niligundua kuwa, ni wale wanaofugwa. Si nilishazoea kila ninapoona nyuki, basi huwa ni wale wa msituni na kufua (kuvuna) unajipangia mwenyewe, lakini kumbe hawa ni wale waliochini ya himaya ya vijana wa kijiji cha Fuuweni shehiani hapo. Sikutaka kuonekana mwizi, la hashaa….nilimvuta kijana mmoja pembeni nikamuuliza, ikiwa wahusika wa wanaofuga mizinga hiyo, wapo karibu ili nizungumze nao. Walishasema wahenga nyota njema huuonekana alfajiri, nami nilibahatika kuzungumza na Msaidizi Katibu wa ushirika huo wa ‘Jambo nia’ Salu...

WAZIRI PEMBE AITANGAAZA KAMPENI YA “MTOTO MBONI YANGU”,

  HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE RIZIKI PEMBE JUMA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUTOA TAARIFA YA KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA “MTOTO MBONI YANGU”, SIKU YA TAREHE 25/10/2024 KATIKA UKUMBI WA WIZARA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO - KINAZINI ZANZIBAR   NDUGU WAANDISHI WA HABARI ASSALAMU ALAYKUM.     Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema ya uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana siku ya leo kwa ajili ya kutoa taarifa ya     KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA MTOTO MBONI YANGU. NDUGU WAANDISHI WA HABARI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto Ajira”   kutoka Dar es Salaam imeandaa kampeni ya kitaifa yenye jina la MTOTO MBONI YANGU , ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Zanzibar.   Lengo kuu la kampeni hii   ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuizunguka nchi nzima ya na kuielimisha, kuiasa na kuzung...

MIEZI 24 YAPOTEZA WATU 3,192 KWA AJILI BARABARANI TANZANIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JESHI la Polisi Tanzania, limesema kuwa, watu 3,192 wamepoteza maisha nchini kote, kufuatia ajali za barabarani, katika kipindi cha kuazia mwaka 2022 hadi Disemba mwaka 2023.   Kati ya hao waliopoteza maisha, watu 1,545 waliripotiwa mwaka 2022 na watu wengine 1,647 waliripotiwa kuanzia Januari hadi Disemba mwaka 2023. Aidha, kwa upande wa Zanzibar, kuliarifiwa kuwepo kwa watu 297 walipoteza maisha, na kati yao mwaka 2022 walikuwa 137 na mwaka 2023 idadi iliongezeka 23, na kufikia watu 160 walipoteza maisha. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za uhalifu na matukio ya usalama barabarani, ya Jeshi la Polisi Tanzania ya mwaka 2023, iliyosainiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Camillus M. Wambura na kuweka kwenye tovuti ya Ofisi ya taifa ya takwimu Tanzania. Ripoti ikaeleza kuwa, watu hao waliofariki, walitokana na matukio ya ajali 3,453 ambapo kati ya hayo, mwaka uliobeba ajali nyingi ni mwaka jana. Ambapo kulikuwa na matukio 1, 73...