Skip to main content

Posts

WIKI YA MWANANCHI, MAMBO NI MOTOOO....MASHABIKI BAGAMOYO WATOA MSAADA WA MADAWATI

  Na Mwandishi Wetu@@@@ Kuelekea wiki ya Mwananchi, Mashariki wa klabu ya Yanga wa Kijiji cha Buma kilichopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  wamejitokeza kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwamo madawati. Mashabiki hao walikabidhi madawati hayo katika  shule ya Msingi Buma iliyopo kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada kwa jamii kuelekea siku ya Mwananchi inayotarajiwa kufanyika Agosti 4 Mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu 'Lupaso'. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Tawi la Buma Ismail Omary amesema kuwa, wanachama  wamekua na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lengo ni kurudisha hisani kwa wananchi wanaowazunguka kutokana na mwendelezo mzuri wa timu yao. " Leo tumejitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi Buma lengo ni kutoa msaada wa madawati ili wanafunzi waweze kuyatumia wakati wa masomo, huu ni utaratibu wetu wa kurudisha fadhira kwa wananchi kutokana na  hamasa tunqzozipata za tim...

'MAREKEBISHO KANUNI ZA MAADILI VYAMA VYA SIASA KUJALI USAWA WA KIJINSIA'

  ZANZIBAR                                                                                             Naibu Msajili wa vyama vya siasa Mohammed Ali Ahmed amesema sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa zinaendelea   kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka usawa wa kijinsia pamoja na kukuza uwajibikaji na kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake ili waweza kushiriki kikamilifu katika siasa na   demokrasia nchini. Akizungumza kwa niaba ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa, Afisa sheria Mwandamizi kutoka ofisi hiyo Abdulrazak Ali kwenye mkutano wa tathmini iliyoangalia vikwazo vinavyowakwaza wanawake katika kugombea na kushiriki masuala ya kisiasa   uliofanyika   ukumbi wa ZURA Maisara mjini Unguja, ambao uliowashirikisha wadau mb...

BONANZA LA MAZOEZI PEMBA: MAKAMU WA KWANZA ATOA RAI KUNDOA DHANA POTOFU MICHEZONI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amevishauri vilabu ya mazoezi nchini, kujitengenezea kanuni, zitakazowavutia watu wingi zaidi kujiunga kwenye mazoezi, ili kuondoa dhama potofu ya mazoezi ni uhuni. Alisema, kama kundi kubwa la watu wanadhana kuwa mazoezi ni uhuni na kuvunja maadili, ni wakati sasa kwa vilabu vya mazoezi na michezo, kuwa na kanuni zitakazofuta dhana hiyo. Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Julai 28, 2024 uwanja wa michezo Gombani Chake chake, kwenye bonanza la miaka 10, tokea kuanzishwa kwa ‘Gombani Fitness Club’ lilioandaliwa kwa pamoja na TAMWA-Zanzibar na Shirika la Bima. Alieleza kuwa, kwa vile mozoezi ni jambo muhimu kwa kila mmoja, ni vyema kuwepo na kanuni ndogo ndogo, ambazo zitawavutia wengine, kushiriki katika kupata kinga ya miili yao. Alifahamisha kuwa, ni kweli kama kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili, inaweza kuwa sababu kwa baadhi ya watu, kuona sio sehemu salama, ingawa ...

IDARA YA KATIBA: ''WANAWAKE MSIOGOPE TALAKA TOWENI USHAHIDI MAHKAMANI'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ IDARA ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, imewataka wanawake wa Junguni wilaya ya Wete, kutoacha kuzisimamia kasi za udhalilishaji hata kama mtendaji ni muume wake, kwa hofu ya kutishiwa talaka. Kauli hiyo imetolewa leo Julai 25, 2024 na Afisa sheria kutoka Idara hiyo Ali Haji Hassan, wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Junguni wilaya ya Wete, kwenye muendelezo wa mikutano ya wazi, ya kuihamasisha jamii, kutoa ushahidi na kuziripoti za kesi za udhalilishaji, ulioandaliwa kwa ushirikiano na Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar. Alisema, kama muume amebainika kwa kosa ubakaji, mwanamke lazima ashirikiane na vyombo vya sheria na kuondoa hofu ya talaka, ikiwa ni njia moja wapo ya kutokomeza matendo hayo. ‘’Hakuna hatia pasi na mwananchi kufika mahkamani kutoa ushahidi, sasa niwaombe wanandoa, wasiogope kuachika na wasimamie haki ya mtoto mahkamani,’’alishauri. Katika hatua nyingine, Afisa huyo sheria, alisema bado jamii haijakuwa...

DODO PUJINI WATOA RAI KUMALIZA UDHALILISHAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Dodo wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema njia moja ya kupunguza matendo ya udhalilishaji ndani ya jamii, ni wakati sasa kwa sheria kubadilishwa, ili mwanamke naye aliyechangia kutokea kwa tendo hilo, atiwe hatiani. Walisema, wapo wanawake wameshasababisha kufungwa kwa wanaume wengi, nae akiendelea na shughuli zake mtaani, jambo ambalo linaweza kuwapoteza wanaume hapo baadae. Wananchi hao, waliyasema hayo leo Juni 24, 2024 Dodo Pujini, wakati wa mkutano, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, kwa kushirikiana na Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, kwa ufadhili wa ‘UNDP’ kupitia mradi wake wa upatikanaji haki Zanzibar. Walisema, bado makosa ya ubakaji yanawaelekea wanaume pekee, hata kama mwanamke mwenye umri unaopindukia miaka 18, nae alichangia kwa njia moja ama nyingine. Haji Shaibu Hamad miaka (70), alisema ubakaji ambao uko wazi ni ule wa mwanamme kumtumia nguvu mwanamke, lakini ule wa kuridhiana ni v...

AFANDI KHALFAN ATIMIZA AHADI KWA WAVUVI

      NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WAVUVI wa bandari ya Tanda Tumbi Shehia ya Mjanaza Wilaya ya Micheweni Pemba, wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya Hali ya Hewa, ili kuweza kujikinga na matatizo yanayoweza kutokea wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi.   Hayo yalielezwa na Mkaguzi wa Polisi ambae pia ni Polisi shehia ya shehia ya Mjanaza Khalfan Ali Ussi, wakati akikabidhi simu kwa wavuvi hao, ikiwa ni ahadi iliyoitoa kwao hivi karibuni.   Alisema, kwa vile wao ni wavuvu anamatumaini makubwa kuwa,   simu hizo lengo lake ni kuwasaidia katika shughuli zao hizo, pindi wanapopatwa na majanga mbali mbali.   Alifahamisha kuwa, lengo la kutoa simu hizo ni kutokana na maafa mbali mbali, ambayo yanawapata wavuvi wakiwa katika shughuli zao, na kukosa chombo cha mawasiliano.   "Leo (jana), nimekuja kwa ajili ya kutimiza ahadi yangu, niliyoiweka kwenu kuwapatia simu ambayo itaweza kuwasaidia, pindi mnapotokezea ka...

BARAZA LA WATOTO WAWI, LAKERWA ADHABU NYEPESI KWA WABAKAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ BARAZA la watoto la shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, limesema bado hawaridhishwi na hukumu nyepesi zinatolewa mahakamani, kwa washtakiwa wanaowabaka watoto na wanawake. Walisema, bado hukumu zinazotolewa na mahakma maalum za kupambana na udhalilishaji, zinawafaidisha wabakaji, jambo ambalo, linatishia kuendelea kwa matendo hayo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema, Baraza la Wawakilishi mwaka 2018, lilipitisha sheria kali kwa watakaotiwa hatiani kwa udhalilishaji, ingawa bado mahakimu hawaitumii ipasavyo. Walisema, wamesomeshwa kuwa, mahkama ikimtia hatiani mshitakiwa kwa makosa ya ukatili na udhalilishaji, adhabu yake ni kuanzia kifungo kisichopungua miaka 30 au maisha, ingawa hakuna aliyetekelezewa adhabu hiyo. Mjumbe wa baraza hilo Aisha Mohamed Juma, aliema anashangaa kuona washtakiwa wanafungwa miaka kati ya 10 au 15 tu, jambo ambalo anashindwa kuwaelewa mahakimu. Alieleza kuwa, hajaona wapi mahak...