NA MWANDISHI MAALUM, @@@@ Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) imefanya ziara mkoani Mtwara na kutembelea miradi ya gesi iliyopo Msimbati na Madimba. Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Ombeni Sefue amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa taifa ambapo asilimia 65 ya gesi hutumika kuzalishia umeme nchini. Amesema kuwa gesi hiyo inatumika kuzalishia umeme nchini ambapo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi. “Tumefarijika kupata fursa ya kuwaonyesha wawakilishi wa wananchi fedha za taifa hili zinavyotumika na mchango inayotolewa katika uchumi wa nchi kama mlivyosikia asilimia 65 ya umeme unaotumika nchini unatokana na gesi asili ya Songosongo na Mnazibay tumekabidhiwa jukumu hili kubwa kwa Taifa” amesema Sefue Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Clement Sangu Mbunge wa Jimbo la Kwela Zanzibar amesema kuwa ziara hiyo ni ziara maalum ya kibunge ambayo imeanzia mkoani Ta...