NA ASIA MWALIM, ZANZIBAR@@@@ NCHI nyingi zimeridhia mikataba na matamko ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kwenye uongozi na nafasi za maamuzi kama ilivyoainishwa katika Tamko la Haki za Binadamu la 1948. Zanzibar imesaini mikataba ya kikanda na kimataifa, lakini safari ya utekelezaji ni ndefu kwa sababu hadhi sawa kwa wanawake na wanaunme katika uongozi haipo na hii inaonekana katika shehia, wadi, majimbo, wadi hata taifa kutokana na kutokuwepo fursa sawa katika kugombea uongozi. Mara nyingi unapofanyika uteuzi nafasi wanazopewa wanawake huwa hazina hadhi sawa na zile wanazokabidhiwa wanaume na hii inapelekea wanawake kuwa na wakati mgumu kufikia malengo yao na ndio maana upo umuhimu wanawake kupaza sauti zao kutaka mabadiliko. Vyama vya siasa navyo vinawaacha nyuma wanawake katika kuwapa nafasi za kugombe ...