Skip to main content

Posts

HAMA HAMA WATUMISHI WA UMMA, IPA YAGUNDUA JAMBO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHUO cha Utawala wa Umma Zanzibar ‘IPA’ kimegundua sababu mbali mbali, zinazowafanya watumishi wa umma, kuhama sehemu moja kwenda nyingine, ikiwemo mabadiliko ya sayansi na teknolojia. IPA imegundua sababu nyingine kuwa ni, miundo ya kiutumishi, maslahi na ndoa kwa watumishi wanawake na wanaume, kwa kumfuata mwenzake sehmu alipo kimakaazi. Hayo yameelezwa leo Disemba 8, 2023, na Mkuu wa Divisheni ya Utafiti na Ushauri Elekezi kutoka ‘IPA’ Haji Jumbe Haji, wakati akizungumza kwenye uwasilishaji wa matokeo ya awali wa tafiti nne walizozifanya, kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Chuo, hicho mjini Chake chake. Alisema, sababu hizo na nyingine, zinazowafanya watumishi wahame kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakati mwingine huathiri mtiririko mzuri wa kazi za sekta ya umma. Alisema, tafiti hizo ambazo walizifanya katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, zilichukua takriban miezi sita hadi kukamilika kwake, ambapo watendaji mbali mbali wa sekta ...

WANAWAKE WAKULIMA WA MWANI PEMBA WAMALIZA MAFUNZO YA KUOGELEA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAWAKE wanaolima na kilimo cha mwani cha kina kirefu, wa kijiji cha Tundaua shehia ya Kilindi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku 15, sasa wanajiamini kuogelea, hadi urefu wa uwanja wa mpira wa miguu bila ya kupumzika. Walisema, mafunzo hayo, yamewajengea uthubutu wa kuogelea na hata kuokoana, pindi ikitokezea ajali wakati wa kwenda ama kurudi kwenye shughuli yao ya kilimo cha mwani, kwenye maji yenye kina kirefu. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwenye bahari ya Tundaua walikokuwa wakifundishwa, walisema kwa sasa wamejitoa woga na wanajiamini kogelea hadi mita 100 (urefu wa uwanja wa mpira wa miguu), bila ya kumpunzika. Walieleza kuwa, wazo lililoibuliwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kipitia Idara ya Mazingira chini ya mradi wa ‘SAPPHIRE’ umekuja kuwapa uhakika wa kazi zao. Mmoja kati ya wanufaika wa mafunzo hayo ambae ni mkulima wa mwani wa kina kirefu, Hassina Seif Baki, ...

WAVUVI WA DAGAA WESHA WATAKIWA KUZINGATIA HILI KWANZA.................

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAVUVI wa dagaa wa shehia ya Wesha wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kujiwekea mazingira ya usafi, kuanzia nguo wanazovaa, madau yao pamoja na vyombo vyingine wanavyotumia, ili kuliongezea thamani dagaa lao. Ushauri huo umetolewa leo Disemba 6, 2023  na Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Jamii kwa kuzingatia Ikolojia na shughuli za kijipatia kipato, kwa wavuvi wadogo katika eneo la hifadhi ya mkondo wa Pemba ‘’SAPPHIRE’ Aisha Abdalla Rashid, alipokuwa akifungua mafunzo, kwa wavuvi hao, yaliyofanyika ukumbi wa Manispaa ya Chake chake. Alisema, kwa sasa ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira, chini ya mradi huo wa ‘SAPPHIRE’ imeamua kukutana na wavuvi na waanika dagaa, ili kujengea uwezo kwa lengo la kuongeza thamani. Alieleza kuwa, moja ya jambo hilo ni usafi wa wavuvi, kuanzia nguo wanazovaa wakati wanapokwenda kwenye shughuli zao za uvuvi, madau yao na ndoo wanazotumia. ‘’Usafi wa bidhaa ya dagaa kavu au bic...

WAANIKAJI DAGAA NDAGONI WAPIGWA MSASA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANIKAKAJI dagaa wa shehia ya Ndagoni wilaya ya Chake chake Pemba, wameshauriwa kuzitumia njia nzuri za uanikaji, ikiwemo kutumia chanja za miti zilizoinuka ‘chanja’ ili kuepusha vumbi na taka taka, zinzoweza kupunguza thamani ya bidhaa hiyo. Walielezwa kuwa, njia nyingine ambayo ni nzuri kwa uanikaji na kutumia sakafu iliyasafi, ambayo ni vyema ikazungumshiwa kinga maalum, ambayo itazuia taka taka na wanyama kuliharibu wakati wa uanikaji. Hayo yamelezwa na Kaimu Afisa Mkuu Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Pemba Mayasa Hamad Ali, wakati akitoa mada njia ya uanikaji bora dagaa, kwa waanikaji na wavuvi wa shehia ya Ndagoni, mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa Manispaa ya Chake chake. Alisema, njia nyingine ambayo waanikaji wanapaswa kuitumia ni kutumia wavu, ambao kitaratibu hutakiwa kuwekwa juu juu, ili kuhakikisha dagaa haliingii wadudu na taka taka. Alieleza kuwa, njia hizo pamoja na ile ya kutumia moshi kwa magamba ya miti maal...

WANAODAIWA KUUA KWA MAKSUDI WAWI, KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WAKIWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa makusdi, inayowakabili vijana wanne akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ na wenzake, wote wakaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake, wamerejeshwa tena rumande, baada ya Jaji anayesikiliza kesi yao kutokuwepo mahkamani. Watuhumiwa wingine waliorejeshwa rumande hadi Januari 23, 2024 ni Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 na Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, ambao wanatuhumiwa kumuua kwa maksudi kijana Said Seif Kombo. Mara baada ya kuwasili mahakamani hapo wakitokea rumande, walitulia tuli wakisubiri taratibu za mahakama kuu ziendelee, ingawa Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Awamu Zubeir Awamu, alidai kuwa Jaji husika hayupo mahakamani hapo. Wakili huyo wa serikali, alimueleza hakimu wa mahkama ya mkoa Chake chake anayeshughulikia makosa ya udhalilishaji Ziredi Abdull-kadir Msanifu, juu ya dharura ya Jaji husika wa kesi hiyo. ‘’Mheshimiwa Hakimu, ilikuwa kesi hii...

WANAWAKE WAWAONESHA WENZAO NJIA KUINGIA KWENYE SIASA, CHANGAMOTO ZIGEUZENI FURSA SAFARI IENDELEE

    NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ UONGOZI ni haki ya kila mtu, awe mwanaume au mwanamke. Tena hapa tunajifunza kuwa, hata kundi la watoto wa kike ama wakiume, wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii yao. Jamii imeshazowea kuona mwanaume ndio anaeweza kuwa kiongozi na kusimamia nchi katika hali zote, kuliko wanawake na hii kutokana na mitazamo yao isijengwa kimamtiki. Ingawa mtazamo huu, unaweza ukaondoka kwasababu mwanamke ameweza kuongoza familia na kuweza   kusimama imara,   kwahivyo hatoshindwa kuisimamia nchi nzima. Mfano hai na wa kweli kwa sasa ndani ya taifa la Tanzania, rais anayewaongoza wananchi wastani wa milioni 60 ni Dk. Samia Suluhu Hassan (mwanamke), na kila mmoja ni shahidi hajatetereka kwenye nafasi hiyo. Tena anasimamia vyema familia yake, pamoja na wananchi wake na kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika nchi na mengi yameongelewa kuhusu yeye bali hakukata tamaa. KWA NINI WANAWAKE HAWAONEKANA KW...