Skip to main content

Posts

MRADI WA ‘SWIL’ ZANZIBAR, ULIVYOWAONESHA NJIA WANAWAKE KUDAI HAKI ZAO: TAMWA, PEGAO ZASEMA JAMBO

                  NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@  HAWAKUKOSEA waliosema 'umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu' Msemo huu umesadiki katika utekelezaji wa mradi wa kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi , demokrasia na siasa 'SWIL' unaotekelezwa kwa mashirikiano kati ya   TAMWA Zanzibar, ZAFELA na PEGAO. Mradi huo ambao ulizinduliwa mwaka 2020 na kutarajiwa kumalizika 2023 umeonekana na mafaniko makubwa katika hatuwa mbalimbali za utekelezaji wake. Utekelezaji wa mradi huo ambao ulitarajiwa kuwafikia na kuwawezesha wanawake 6000 kwa zanzibar, Unguja na Pemba katika kudai haki zao ili nao waweze kuwawezesha wengine tayari umeonyesha njia katika kufikia hatuwa ya kudai haki zao za uongozi.   Mradi huo wa SWIL ambao unafadhiliwa na ubalozi wa Norway umetekelezwa maeneo mbalimbali ambapo kwa upande wa   Pemba tayari     umeshawafikia wastani wa wanawake 4000.   Katika hatuwa za kufanikis...

RAIS MAHKAMA YA AFRIKA AWAPA NENO WANAOWAKINZA WAANDISHI

  NA HAJI NASSOR, ARUSHA RAIS wa Mahkama ya Afrika ya haki za binaadamu na haki za watu Imani Daud Aboud, amesema kama waandishi wa habari wanafanyakazi zao chini ya vitisho kutoka kwa mamlaka kunahatarisha kudhoofisha uhuru wao na ule wa kujieleza na kutoa maoni. Rais huyo aliyasema hayo jana ukumbi wa mahakama hiyo mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa kikanda kwa waandishi wa habari juu ya ulinzi na usalama wao uliondaliwa na Baraza la habari Tanzania MCT. Alisema vipo vyombo au mamlaka vimekuwa vikiingilia na kuwatisha waandishi wa habari wanpokuwa kazini jambo ambalo halisidii kuimarisha uhuru wa kujieleza na ule wa habari. Alieleza kuwa,  haki ya kupata na kusambaaza habari ni haki ya kikatiba hivyo ni kosa kwa mamlaka nyingine kuviingilia vyombo vya habari pasi na dai la haki. 'Waandishi wa habari ni sauti ya wsiokuwa na sauti na ni sauti kwa waliokata tamaa hivyo ni jukwaa muhimu na linapaswa lilindwe na sio kushambuliwa,'alieleza. Katika hatua nyingine rais huy...

KAMANDA MCHOMVU AWAPA NENO WAZAZI

  KAMANDA   wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kamishina Msaidizi wa P olisi Richard (ACP), Thadei Mchomvu, amewataka wazazi na walezi   kushirikiana kwa pamoja katika kuwalea na kuwatunza watoto wao kwa ajili ya kuwalinda    na vitendo vya ukatili na udhalilishaji. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake Muembe Madema M jini Zanzibar, amesema baadhi ya wazazi   hushughulikia   shughuli zao zaidi na hawana utamaduni wa   kuwa   karibu na watoto wao jambo ambalo hupelekea kuendelea vitendo hivyo. "Wapo wazazi wakitoka asub u h i ndo wametoka kurudi kwao ni usiku watoto wakiwa wamelala, mtindo ambao unachangia watoto kukosa elimu ya kujitambua   iliyo muhimu katika kuwasaidia kuepuka kufanyiwa vitendo viovu vya kudhalilishwa," a lisema Richard " Na baadhi ya kina mama wanawacha watoto kudhurura ovyo bila ya kuwavisha nguo kamili na kupelekea mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji." Aliongezea Richard Aid...

WANACHAMA WAMCHAGUA TENA MLAY KUWA RAIS MCT

    NA HAJI NASSOR, ARUSHA@@@@ WANACHAMA wa Baraza la Habari Tanzania MCT, wamemrejesha tena Rais wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Juxon Isaac Mlay kwa miaka mengine mitatu ijayo, kupitia mkutano mkuu wa 25, uliofanyika Septemba 28, 2023 mkoani Arusha. Mkutano huo, pia umemchagua Yussauf Khamis Yussuf kuwa Makamu wa rais   na wingine waliochaguliwa katika mkutano huo ni wawakilishi wa vyombo vya habari, akiwemo Tido Mhando. Wawakilishi wingine ni Rose Rouben, Ali Haji Mwadini samba mba na kupatikana kwa wawakilishi watatu, kundi la umma wakiongozwa na CPA: Happiness Nkya, Jaji Robert Makaramba na Mwajaa Said. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, rais aliyerejea tena madarakani Juxon Isaac Mlay, alisema kasi na ari iliyokuwepo kwa miaka mitatu, ni vyema ikaongezeka. Aliwataka viongozi wenzake, waliorudi kutetea nafasi zao, kuhakikisha wanaendelea kufanya makubwa, wakiwa ndani ya Baraza la Habari Tanzania, ili kuwalipa wanachama waliowachagua. ...

MAKTABA ZA SKULI ZIWE CHEM CHEM YA UFAULU KWA WANAFUNZI

             NA TATU NAHODA, ZU@@@@ ……………fuata nyuki ule asali……………. Ndivyo walivyosema wahenga, wakimaanisha kuwa, unapaswa kufuata vitu, watu au sehemu zenye ujuzi, ili kufanikiwa katika malengo yako.   Msemo huu unatumika katika nyanja nyingi ikiwemo ya wanafunzi wanaofuta elimu, hasa kwa mfumo wa kupitia maktaba ziwe na skulini au maeneo mingine. Maktaba ni hazina pekee inayomtajirisha mwenye kuhitaji utajiri wa kitaaluma na kimaarifa, kwani mtumiaji hapitwi na wakati, na hupata taarifa muhimu juu ya mambo mbali mbali. Kwa wanafunzi na walimu wao, maktaba imekuwa ni hazina yao ya thamani, kama alivyosema mtaalamu Marcus Tallus Cicore " if you have a garden and library you have everything you need " ukiwa na tafsiri   isiyorasmi kuwa, kama una bustani na maktaba basi tayari una kila kitu. KWANINI MAKTABA NI MUHIMU SKULINI? Ahmed Khamis Ahmed mwanafunzi wa kidato cha pili skuli ya Madrasatul-Ahbaab Kisauni Unguja anasema, m...

WANAOKULA DAWA KWA KUJIKADIRIA WENYEWE WAJICHIMBIA KABURI TARATIBU

    NA MOZA SHAABAN, ZU@@@@ KILA siku mwanadamu amekuwa akihangaikia afya yake na ustawi wake. Kwa karne zilizopita, mwanadamu alitumia mimea, mboga mboga na wanyama, ili kuponya magonjwa na maradhi mbali mbali yaliokua yakimsibu. Kwa vile wakati haugandi, sayansi inayochunguza faida na athari za vitu vya kemikali, kwa matibabu au kuzuia magonjwa, kupunguza maumivu na nyenginezo ilizuka. Na hapa dawa mbali mbali ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binaadamu, zilianza kutengenezwa hususan zile za kemikali, ili kurekebisha au kuboresha hali ya afya ya mtu. DAWA NI NINI ? Dawa za binaadamu ni kitu chochote, ambacho binaadamu anatumia kwa lengo la kutibu au kukinga maradhi yasishambulie kinga za mwili. Zinaweza kuwa katika aina tofauti, kama vile vidonge, sindano, matone, creams au loshan pamoja na za unga unga. Kwa mfano, dawa za antibiotics hutumiwa kutibu maambukizi ya bakteria, za antiviras hutumiwa kutibu maambukizi ya virusi, na dawa za analgesic hutumiwa ku...