Skip to main content

Posts

JACKLIE "INTERNEWS KUENDELEA KUWANOA WAANDISHI TANZANIA"

                                                      NA HAJI NASSOR, PEMBA MKUU wa mradi jumuishi wa vyombo vya habari kanda ya Afrika kutoka shirika la kuwajengea uwezo waandishi wa habari Jacklie Jidubwi, amesema shirika hilo litaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuwa waledi kwa kuibua maumivu yanayowakumba watu wenye ulemavu chini. Mkuu huyo wa mradi aliyasema hayo machi 8, mwaka 2022 mjini Zanzibar wakati akiyaghairisha mafunzo ya siku2 kwa wanahabari wa Zanzibar juu ya uandishi bora wa habari za watu wenye ulemavu kupitia mradi wa jumuishi wa vyombo vya habari. Alisema Internews imevutiwa mno na kazi na mwamko walionao waandishi wa habari wa Tanzania wakiwemo wa Zanzibar kwa kuibua changamoto na madhila yanayowasakili watu wenye ulemavu. Alieleza kuwa kwa juhudi hizo za wazi wazi ndio maana shirika hilo limevutiwa na kazi hizo na kua...

Tukiwapa uongozi wanawake sio hidaya ni haki yao kikatiba

                                                NA HAJI NASSOR, PEMBA INAWEZEKANA wapo wanaodhani kuwa suala la kumpa uongozi mwanamke, kuanzia shehia hadi taifa, ni kama hidaya kutokwa kwa wenye mamlaka. Hidaya ni zawadi ambayo inawezekana mtu asipewe au pewe kwa mtoaji akiona ipo haja hiyo. Na wale wenye mamlaka na uwezo wa kushawishi mwanamke kupata nafasi ya uongozi, hudhani kuwa hili ni hidaya. Maana utasikia kauli kutoka kwa viongozi wanaume wakisema kuwa, kamati ya shehia fulani kama ina wajumbe 12, basi angalau wanawake wawe watatu. HALI HALISI Wanawake wanasema wamekuwa wakishuhudia kauli za kukatisha tama kuwa, hutumika maneno kama vile angalau wanawake wawili, lazima wanawake waepo. Asha Hassan Omar wa mtandao wa wanawake Mkoani anasema, imekuwa kama zawadi kutokana kwa wanaume wanapotaka kupewa nafasi. Anasema kwa karne hii tayari wameshapa uwelewa wa jinsi...

WAZIRI SAADA MKUYA ALIA NA MIUNDOMBINU ISIYORAFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

  NA HAJI NASSOR, PEMBA WAZIRI wa nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar dk. Saada Mkuya Salim amesema bado watu wenye ulemavu wanaendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo wanaofika baraza la wawakilishi kwa shughuli mbali mbali. Dk. Saada Mkuya aliyasema hayo Machi 7 mwaka 2022 ukumbi wa hoteli ya Maru maru mjini Zanzibar alipokuwa akifungua mafunzo ya siku2 ya uandishi wa habari za watu wenye ulemavu yalioandaliwa na Shirika la Internews kupitia mradi wa vyombo vya habari jumuishi nchini. Internews in Tanzania Alisema muhimili wa baraza la wawakilishi lilipaswa kuwa mfano mzuri wa kuweka miundombinu rafiki kwa kundi la watu wenye ulemavu ili iwe rahisi kwao wanapowagania haki zao. Alieleza kuwa hivi karibuni alimshuhudia mwanamke aliyealikwa barazani hapo akibebwa na wanaume ili kufika juu sehemu ya wageni. Internews Aidha Waziri huyo aliipongeza Internews Tanzania kwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuibua changamoto za watu wenye ulemavu Zanzibar...

UTALII WA VISIWA VIDOGO VIDOGO MKOMBOZI WA UCHUMI KWA WANANCHI

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA SERIKALI ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Hussen Ali Mwinyi imelichukua suala la uwekezaji wa visiwa vidogo vidogo Zanzibar katika hatua nyengine ambayo ni nzuri na yenye manufaa kwa nchi. Agosti hadi Septemba mwaka 2021, Serikali ilitangaza awamu ya kwanza ya uwekezaji, ambapo visiwa vinane (8) vilipata wawekezaji kati ya kumi (10) vilivyotangazwa. Visiwa hivyo ni Changuu, Pwani, Bawe, Pamunda A na B, Kwale, Chumbe, Misali, Njau na Matumbini A, ambapo kisiwa cha Njau na Matumbini A wawekezaji walishindwa masharti. Serikali imeweka vigezo maalumu kwa wawekezaji wa visiwa na ikiwa hakufikia, hatopatiwa kwani Serikali iko makini kwenye suala hilo. Anasema Mkurugenzi Uwekezaji Pemba Al-haji Mtumwa Jecha, awamu ya pili ilitangazwa mwaka huu, ambapo kwa Pemba ni kisiwa cha Matumbini, Jombe na Kwata Kusini na Kashani, Njau na Fundo Kaskazini.    Visiwa hivyo vitakodishwa muda mrefu ili vijengwe hoteli za kitalii zitakazotoa huduma mbali m...

KIKUNDI CHA 'KHERI LIWE" KENGEJA WAANZA KUONA MWANGA, WAIPA TANO TAMWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KIKUNDI cha ‘Kheri liwe’ kilichopo Likoni shehia ya Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, kimesema mafunzo, mawazo na fikra walizopewa na TAMWA-Zanzibar, sasa zimezaa matunda baada ya kujipatia zaidi ya shilingi milioni 2.8 ikiwa ni faida kwa miaka mitatu iliyopita. Wanakikundi hao, walisema baada ya kuanzisha mpango wa kuweka fedha na kukopa ‘ hisa ’ ambao walishawishiwa na TAMWA, na kufanya biashara ndogo ndogo, utengenezaji sabuni na kilimo cha mboga, sasa wameona matunda yake. Wakizunguma na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, wanakikundi hao, walisema kumbe walichelewa kujikusanya na kama wengeanza miaka ya nyuma zaidi, kwa sasa wengeshapiga hatua kubwa zaidi. Walieleza kumbe zipo fursa kadhaa endapo jamii itazifanyiakazi kupitia vikundi hivyo, na kisha kuwezeshwa kimafunzo na fikra za jinsi ya kukusanya fedha na kisha kujikopesha wenyewe. Mwenyekiti wa kikundi hicho Fatma Nahoza Juma, alisema sasa kila mwanachama ameshapata faida, iwe wakati w...

POLISI KASKAZINI PEMBA LAMDAKA KIJANA NA MISOKOTO 60 BANGI

  NA ZUHURA   JUMA, PEMBA JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limemkamata kijana Hemed Omar Ali mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Konde Chanjaani baada ya kupatikana na misokoto 60 ya dawa za kulevya aina ya bangi yakiwa nyumbani kwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis alisema, mtuhumiwa huyo amekamatwa Febuari 6 mwaka huu majira ya saa 9:30 jioni huko nyumbani kwake Konde Chanjaani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba alipatikana na misokoto 60 ya bangi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda huyo alisema, mtuhumiwa huyo ni maarufu kwa uuzaji wa madawa ya kulevya, hivyo Jeshi la Polisi limemshikilia baada ya kufanya operesheni katika maendeleo mbali mbali ya Mkoa. “Pamoja na Jeshi la Polisi kufanya msako katika maeneo yote ya Mkoa, lakini walikuwa hawajafanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, kwa bahati nzuri tulimkamata na tunaendelea mahojiano”, alieleza Kamanda huyo. Kamanda Sadi alieleza kuwa, upelelezi wa kesi hiyo unaen...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

IRELAND YARIDHISHWA UTEKELEZAJI MRADI WA ARDHI PACSO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA NAIBU Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mags Gaynor, ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa umiliki wa rasilimali ardhi kwa wanawake, uliokuwa ukitekelezwa na Mwemvuli wa asasi za kirais Pemba ‘PACSO’ na kumalizika hivi karibuni. Naibu Balozi huyo alisema, kutokana na majibu ya wanufaika wa mradi huo alivyozungumza nao, ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, na hasa kwa kuwafikia walengwa. Alisema mradi huo ulilenga kuwafikia wanawake ili kuwajengea uwelewa, juu ya umilikiwa wa rasilimali ikiwemo ardhi, jambo ambalo sasa, limewanufaisha hasa kwa kuwepo wanufaika waliopata haki zao. Naibu Balozi huyo aliyasema hayo ofisi za PACSO Chake chake Pemba, kwenye kikao cha tathimi kilichojumuisha wanufaika wa mradi wa uongozi wa PACSO. Alieleza kuwa, kwa vile wapo wanawake kisiwani Pemba walionufaika moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kurithi, kununua ardhi na kulalamikia ucheleweshaji urithi ni hatua kubwa. “Serikali ya Ireland, imeridhishwa mno na mr...