Skip to main content

Posts

TAMWA -ZANZIBAR "SHERIA, SERA ZINAZOLENGA KUPUNGUZA UDHALILISHAJI KWA WATOTO ZITUPIWE JICH0"

  Na Najjat Omar – Unguja.   Wadau wa masuala ya kijamii na kijinsia wamekutana kwa pamoja kuzungumzia sera na sheria zinahusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na mapungufu yake.   Mkutano huo ambao umeendaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar –TAMWA uliokutanisha wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali za kijamii na kiserikali kujadili juu ya ufuatiliaji,utekelezaji na kutoa maoni juu sera na sheria zinahusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa jamii hususan watoto.   Takwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali inaonesha matukio hayo yameongezeka kutoka matukio 1,222 mwaka 2021 hadi matukio 1,360 mwaka 2022, ongezeko ambalo ni la matukio 138.   Takwimu hizo zinaonesha kwamba kwenye matukio 1,361 yaliyotokea mwaka 2022, matukio 1,173 yalijumuisha watoto, 185 yalihusu wanawake na matatu yalihusu wanaume. Kwenye matukio 1,173 ya watoto, 889 walikuwa ni wasichana, huku 284 walikuwa ni wavulana.   Akifungua mkutano huo Afisa miradi ...

TAMWA CHAWAKUTANISHA WADAU WA TEKNOLOGIA NAMNA YA KUPUNGUZA UDHALILISHAJI

    Na Najjat Omar – Unguja.     Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar –TAMWA, wamewakutanisha wadau mbalimbali katika kujadili masuala ya ukuaji wa teknolojia kwenye dhana ya kupunguza vitendo vya udhalilishaji.   Majadiliano hayo yalifanyika katika ukumbi wa Raha Leo ulipo kisiwani Unguja kwa kuwakutanisha wadau wa masuala ya kijamii kama viongozi wa kisiasa,walimu,wanafunzi, viongozi wa dini,Jeshi la Polisi,Mahakimu pamoja wadau kutoka Mahakamani.   Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA –Zanzibar Asha Abdi amesema licha ya ukuaji wa teknolojia kurahisisha masuala ya ujifunzaji kwa watoto ila kwa   upande mwengine unachochea udhalilishaji wa watoto kuiga hata kufanya na kujifunza mambo mabaya.   “Ukuwaji wa teknolojia umekuwa mkubwa ambapo nao una changamoto zake ,watoto wanajifunza mambo huko kwenye mitandao na kujaribu kwa kufanya sasa hii teknolojia pia inachochea sana masuala ya udhalilishaji ...

'WAHARIRI MASHINE NYOOFU UKUZAJI, UIMARISHAJI LUGHA YA KISWAHILI'

  NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIAR   JUHUDI za wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuleta mabadiliko katika matumizi  ya Kiswahili fasaha na sanifu nchini. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika Mkutano wa wahariri wakuu wa vyombo vya habari  kuelekea maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani uliofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.  Amesema wahariri wakuu wana jukumu la kupitisha na kuweka sawa maandishi yote ndani ya Vitabu, Magazeti na majarida hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza lugha ya kiswahili . Aidha  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wahariri kulinda Maadili ya kazi zao katika kuyaibua mambo mbali mbali yasiyoendana na mila, tamaduni na silka zetu bila ya kumuonea Mtu au Taasisi fulani. Sambamba na hayo Mhe. Hemed  ameeleza kuwa kuna fursa nyingi zinazopatikana katika lugha ya K...

WAJASIRIAMALI WATAKA MITAJI KUPIGA HATUA

  NA KAIJE SALIM, ZANZIBAR@@@@ Wajasiriamali wameomba kupatiwa mitaji ili waweze kujikwamua kutoka katika hali moja ya kimaisha na kuelekea kwenye hali nyengine ya kipato cha juu. Ombi hilo limetolewa na wajasiriamali walioshiriki katika mafunzo yaliyo tolewa na SMIDA huko Maruhubi chuo cha utalii. Miongoni mwa washiriki hao ni Aisha Said Omar  wameeleza wamekuwa wakishindwa kujikwamua kimaisha kutokana na mitaji midogo waliyonayo. Chales Silima kutoka kutoka Mamlaka ya mitaji  na dhamana amesema wamekuja Zanzibar kutoa elimu ili wafanya biashara na wajasiri amali wapate kujiendeleza zaidi Amesema mafunzo hayo yatawawezesha hasa vijana kuanzisha majukwa yakujiendeleza kibiashara na kujiwezesha  kufikia katika kuongeza kipato. Kwa upande wake mkurugenz mkuu  Wakala wa maendeleo ya Viwanda vidogo na vyakati SMIDA Soud Said Ali amesema wataendelea kushirikiana wajasiri amali kwa kuwapatia mafunzo iliwapate kufanya kazizao za uzalishaji kwa usahi na kufikia malengo ...

WADAU WA KUPINGA UDHALILISHAJI WALIA UTOROSHWAJI WATUHUMIWA PEMBA

  NA HANIFA SALIM, PEMBA@@@@ WADAU wa Kamati ya kupinga udhalilishaji Kisiwani Pemba wamesema, kukimbizwa kwa watuhumiwa hususani kesi za wanafamilia, ni moja ya changamoto zilizopo zinazorejesha nyuma juhudi zao za kupunguza matendo hayo. Waliyasema hayo katika kikao kazi cha kuwasiliasha ripoti kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu kwa kamati za kupinga udhalilishaji Kisiwani humo, kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Mkanjuni Chake chake. Afisa ustawi wa Wilaya ya Wete Salma Saleh Hamad, akiwasilisha ripoti ya udhalilishaji wa wanawake na watoto kwa kipindi cha miezi sita, alisema kuchelewa kwa kipimo cha DNA na rushwa muhali bado pia ni changamoto kubwa kwa jamii.  Alisema, malalamiko 64 ya matunzo na mvutano wa malezi yaliripotiwa katika kitengo cha ustawi wa jamii, ikiwemo 39 ya matunzi ya watoto na 25 ni mvutano wa malezi, ambapo malalamiko hayo yalipatiwa ufumbuzi na mawili yanaendelea kusikiliza katika ofisi zao ...

MCT KUTAANGAZA WATEULE WA EJAT 2022 WIKI HII

  Majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2022, yanatarajiwa kujulikana Juni 23, 2023 katika kikao kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na waandishi wa habari kitakachofanyika katika ukumbi wa hotel ya The Diplomat ya jijini Arusha. Katika mashindano hayo, jumla ya kazi 893 ziliwasilishwa kutoka vyombo vya habari vya magazeti, radio, runinga na vyombo vya habari vya mtandaoni. Jopo la majaji saba, wenye utaalamu katika habari radio, runinga, magazeti na vyombo vya habari vya mtandaoni walifanya kazi kwa siku tisa ili kupitia kazi hizo. Majaji hao wakiwa chini ya Mwenyekiti, Mkumbwa Ally walifanya kazi hiyo kuanzia Juni 10 mara baada ya kuapishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la  Habari Tanzania (MCT) Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba  Juni 9, 2023. Jopo hilo lilikuwa na wajumbe wafuatao Rose Haji Mwalimu, Mbaraka Islam, Peter Nyanje, Nasima Chum, Dk. Egbert Mkoko na Mwanzo Millinga aliyekuwa Katibu wa jopo ...

WAANDISHI WA HABARI 272, VYOMBO VYA HABARI 94 VYAKUMBWA NA MADHILA TANZANIA

  Ikiwa ni miaka 30 tangu Mei 3 ya kila mwaka ilipotangazwa kuwa siku rasmi ya kuadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) mwaka 1993, matukio mengi ya madhila dhidi ya uhuru wa waandishi na vyombo vya habari hapa nchini yameendelea kutotolewa taarifa. Waandishi wa habari wamechukulia kukumbana na madhila kama unyanyaswaji, kupigwa, kunyang’anywa vifaa, na kutishiwa kama ‘ajali kazini’ na hivyo kutoyatolea taarifa. Msukumo wa taarifa umekuwa ukiwekwa kwenye matukio makubwa yanayohusisha kujeruhiwa, kutekwa ama kupoteza maisha; hivyo taarifa nyingi za madhila hazipo kwenye kumbukumbu.   Uanzishwaji wa Kanzidata na Malengo yake Kutokana na changamoto hii, mwanzoni mwa mwaka 2012 Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilianzisha kanzidata ya kitaifa kwa ajili ya kurekodi  madhila wanayopata waandishi wa habari ama vyombo vya habari. Lengo likiwa ni kuwa na ushahidi wa kitakwimu na uhalisia kwa ajili ya kufanya uchechemuzi  ...

MTAMBWE KUSINI MAJI 'BWERERE', ZAWA YASEMA JAMBO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mtambwe kusini wilaya ya Wete Pemba, wamesema kwa sasa huduma ya maji safi na salama katika vijij vyao, inapatikana kwa urahisi, tofauti na hapo zamani. Walisema, kwa sasa wamekuwa na wakati mzuri wa kujipangia shughuli zao mbali mbali za kimaisha, na wala upatikanaji wa huduma hiyo, sio changamoto inayowatengulia rataiba zao za kimaisha. Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo, walisema kwa sasa huduma hiyo, iko karibu vijiji vyote, tena bila ya mgao, jambo ambalo limechangia kufikia malengo yao. Walieleza kuwa, upatikanaji wa huduma hiyo kwa miaka minne mfululizo sasa, unawapa uhakika wa maisha yao, hasa kwa vile kila mmoja, anaendesha shughuli zake kwa urahisi. Salma Hamad mkaazi wa kijiji cha Kivumoni, alisema kwa sasa huduma hiyo iko vyema na haina shida kwao, ikilinganisha na miaka 20 iliyopita. ‘’Awali sisi wananchi wa kikijiji cha Kivumoni shehia ya Mtambwe kusini, tukifuata maji masafa ya m...

MKAMA NDUME: MTAWALA MBABE PEMBA KIFO CHAKE KIZUNGUMKUTI HADI LEO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ HAPO zamani Magofu ya Mkama Ndume yalikuwa makaazi ya waswahili, ya enzi za kati, ambayo yaliachwa na wakaazi wake katika karne ya 16.   Ambapo hapo, ilikuwa ni kabla ya Wareno Afrika Mashariki inajulikana kwa uimarishaji wake kwa kutumia mawe. Magofufu hayo yako wastani wa kilomita 10 kutoka katikati ya mji wa Chake chake, ambao ndio makao makuu kwa kisiwa cha Pemba.   Kwa wakati huo mji huo ulitawaliwa na kiongozi mmoja aitwaye Mohammed bin Abdul -Rahman, ambaye alijulikana sana kwa ukatili wake kwa raia wake. Na kwa wakati huo alipewa jina la utani la Mkama Ndume lenye maana ya  mkamua wanaume  kwa lugha ya kiswahili cha zamani. Ndio maana, hadi leo eneo hilo lililojaa historia sio kwa kisiwa cha Pemba pekee, bali baraza zima la Afrika na duniani, pakaitwa Mkama Ndume. Kwa kuwa mtawala alikuwa akifanya ibada, alijenga msikiti wa asili wa Ijumaa, miaka 700 iliyopita, ambao ulikuwa na nguzo...