Skip to main content

Posts

HIVI NDIVYO KILIMO MSITU KINAVYOKUWA RAFIKI WA KARIBU KWA UCHUMI WA WANAWAKE

  HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ ‘UKIMUELIMISHA mwanamke umeielimisha jamii nzima' Kutokana na msemo huo, inadhihirika kuwa mwanamke ni muhimili mkubwa, katika dunia hasa pale anapoonekana kuwa na nafasi kubwa ya ulezi ndani ya familia. Ingawa haimaanishi kwamba, baba si muhimu hapana nae ana umuhimu wake mkubwa tu, lakini kwa upande wa mama anaechukuwa nafasi ya ulezi wa familia ni jambo kubwa. Na ndio maana, inafahamika kuwa dunia isingeweza kuendelea mbele bila ya uwepo wa wanawake, kwani kuwekeza kwa wanawake na wasichana kunaleta matokeo makubwa.  Wanawake wanahitaji kuwa na nyenzo madhubuti zitakazowawezesha kuyamudu maisha yao na kuondokana na utegemezi, ambao unaweza kuwa kikwazo katika kuendeleza mbele maisha yao. Pamoja na kuwepo mafanikio na juhudi za wanawake katika sehemu mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, na kijamii bado inaonekana suala la mabadiliko ya tabianchi, linaendelea kuwa na madhara makubwa kwa wanawake.  Wanawake wanazidi kuonekana kama watu walio kat...

BIMKUBWA: MUANZILISHI MPIRA WA PETE WETE, AELEZEA ALIVYOPAMBANA NA DHANA POTOFU

    NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ ‘TULIANZISHA  mchezo huu tukiwa tunajiamini huku  tukijuwa  kuwa na sisi wanawake tuna haki ya kujishirikisha katika michezo ya aina mbali mbali’.    Hayo ni maneno ya kocha wa mpira wa pete timu ya Mchanaga mdogo Center Bimkubwa Maulid Othman, aliyezungumza na makala haya.   Kocha Bimkubwa aliyasema maneno hayo huko katika maeneo ya skuli ya Mchangamdogo Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba, ambapo ndipo wanapofanyia mazoezi.   Akinisimulia miongoni mwa sababu ya kuanzisha mchezo huo, ni pamoja na kuwa michezo ni ajira, afya na kupata kujuwana na watu.    Ingawa anasema alianza kuupenda mchezo huo tokea akiwa mwanafunzi na alikushaanza kuucheza ila kuna kipindi, alisita japo kama ndoto yake ni kuwa mwanamichezo.   Anasema kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo jamii kuwadharau na kuwaona hawafanyi kitu cha maana, na kudai michezo si kwa wananwake, ilibidi avunjike moyo na kukaa tu.   “Tokea tuanzi...

WANANCHI UWANDANI WAKIPA ‘KONGOLE’ ZLSC

   NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, wamesema kambi ya siku tatu ya kutoa ushauri na msaada wa kisheria, inayoendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, imezaa matunda kwao, kwa kupata ufumbuzi baadhi ya changamoto za kisheria, ikiwemo mirathi. Wakizungumza na blog ya Pemba today, leo April 14, 2025  kwenye kambi hiyo skuli ya Uwandani, walisema wamepata ufumbuzi mkubwa, ambao baadhi yao walishakata tamaa. Mmoja wa wananchi hao, aliyekataa kutaja jina lake, alisema tatizo lake la mirathi wa mali kadhaa, umepatiwa ufumbuzi wa haraka, baada ya kuitwa upande anaoulalamikia. Nae Riziki Abdalla Suleiman (29), ambae alilalamikia kukosa vitambulisho vya mkaazi, cha taifa na cheti cha kuzaliwa, sasa amepata muelekeo. ‘’Nilishahangaika kwa zaidia ya miaka 19, lakini sijafanikiwa, ingawa kupitia ushauri wa kisheria uliotolewa na ZLSC, sasa nimeondoka na furaha,’’alieleza. Kwa upande wake Mwana Said Khamis (30), alieleza kuwa,...

‘ZLSC’ CHAPIGA KAMBI YA SIKU TATU UWANDANI CHAKE CHAKE

   NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’, kimewakaribisha wananchi wa shehia za Uwandani wilaya ya Chake chake, kufika ofisini kwao, kwa ajili kupatiwa ufumbuzi wa migogoro mbali mbali ya kisheria, kama vile ya ardhi, tena bila ya malipo. Kauli hiyo imetolewa leo April 13, 2025 na Mwenyekiti wa kituo hicho Pfro: Chris Maina Peter, alipokuwa akizungumza na wananchi hao, kwenye kambi maalum ya siku tatu inayoendelea skuli ya Uwandani. Alisema, kituo hicho hakijasita kutoa ushauri, elimu na msaada wa kisheria bila ya malipo kwa wananchi wasiokuwa na uwezo, kwani sio muda wa kukaa kinyonge kwa wananchi. Profesa Chris, alisema bado mpango wa kituo hicho ni kuendelea kuwasaidia wenye changamoto kama za kukoseshwa vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na fidia kwa ardhi zao. ‘’Ni kweli leo tupo hapa shehia ya Uwandani kwa muda wa siku tatu, tumewafuata wananchi lengo ni kuwasikiliza ikiwa wanachangamoto za mambo ya kisheria, kuwasaidia bila ya malipo,’’alifa...