NA HAJI NASSOR, DAR-ES SALAAM@@@@ WANACHAMA wa Baraza la Habari Tanzania MCT, wamemchagua Rais mpya wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Bernad Luanda, kupitia mkutano mkuu wa 26, uliofanyika Septemba 27, 2024 ofisi za ‘MCT’ Tegeta nje ya jiji la Dar-es Salaam. Kati ya wanachama hai 29, waliohudhuria mkutano huo, waliomchagua rais huyo ni wanachama 27, kura moja ikimkataa na moja iliharibika, ambapo kisha Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Nicholaus Mwaibale alimtangaaza. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Katib Mtendaji mpya wa baraza hilo Ernest Sungura, alisema kwa sasa baraza linakuja kivingine, lengo likiwa ni lile lile la kuwanoa waandishi wa habari. Alisema, kuanzia mwakani, MCT itakua na mradi mkubwa unaojulikana kwa jina la ‘WAJIBIKA’ ambao utakuwa wa miaka saba. Alisema, mradi huo wa paund milioni 30, utagusa karibu kila eneo, ikiwemo kuwajengea uwezo hata waandishi wa habari mmoja mmoja, kupiti vyombo vyao. Alieleza kuwa, jingi...