Na Nafda Hindi, ZANZIBAR Mkurugenzi wa chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa amesema kujitoa na kufanya kazi kwa bidii ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuendeleza na kuimarisha Taasisi kusonga mbele kimaendeleo. Dkt Mzuri amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kuwatambulisha wanachama wapya waliopitishwa kwenye mkutano Mkuu wa mwaka 2024 kwa lengo la kuongeza utetezi wa haki za wanawake na watoto kupitia vyombo vya habari. Amesema Taasisi ili iweze kusonga mbele kimaendeleo inahitaji mashirikiano ya pamoja na uwajibikaji jambo ambalo linaweza kuleta mustakbali mwema kwa Taasisi, mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. “TAMWA ZNZ ilisimama kwa kujitoa sisi wanachama, tumeanzisha jengo letu jipya kwa kukatwa mishahara sisi wenyewe,” Dkt Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA ZNZ. Nae Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ Asha Abdi amewahimiza wanachama hao kulipa Ada ya Uanachama kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kus...