NA HANIFA SALIM, PEMBA:: ‘ ’KIJANA ni mtu yeyote mwenye umri wa miaka 15 hadi miaka 35,’’ndivyo sera na sheria ya vijana Zanzibar inavyofafanua. Lakini kwa upande mwengine kijana ametafsiriwa kuwa ni mwanamke au mwanamme yeyote mwenye miaka katia ya 15 hadi 24, kama sera ya taifa ya Maendeleo na vijana ya mwaka 1996, na kama ilivyorekebishwa mwaka 2007. K ijana ni mtu muhimu kwa taifa lolote ulimwenguni, kwani ndio nguvu kazi ya taifa, ndio taifa la kesho kama wasemavyo baadhi yao. Lakini kijana ndio tumaini la taifa na ndio mtu anayetazamiwa kwa mapana ya nchi, katika kuongoza, kukuza uchumi na kuzima majaribio ya kihalifu. Vijana wanakumbana na changamoto mbali mbali katika maisha yao, na mwisho wa siku taifa linamchukulia kama mtu aliyeshindwa na asiye na msaada wowote kwa taifa lake. Lakini katika umri huo wa ujana, inampasa kijana kujitambua ili aweze kuwa na muonekano halisi, sio kwa umri tu bali matendo zaidi. Ni lazima awe na ushawishi katika masual...