Skip to main content

Posts

WADAU WALIA NA SHERIA TUME YA UTAANGAZAJI ZANZIBAR

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ SASA ni miaka 26 tokea kuasisiwa kwa sheria ya Tume ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997, licha ya kujumuisha na marekebisho yake. Sheria hii, imekuja kusimamia, kuangalia mwenendo wa vyombo vya habari Zanzibar hasa redio, televisheni na vile vya kisasa vyenye kurusha maudhui yao mtandaoni. Sheria hii yenye vifungu 30, vilivyobebwa na sehemu sita kuu, inavyovifungu kwa hakika sio rafiki, kuelekea uhuru kamili wa habari hapa Zanzibar. SHERIA KWA UJUMLA Kama ilivyo sheria nyingine zote, kwenye sehemu ya kwanza imeundwa na vifungu vitatu, maana kile cha nne, kimefutwa na kati ya hivyo kimoja kinatoa jina la sheria na maana ya maneno. Kwa mfano,  mtangaazaji ni mtu ambaye amepewa leseni chini ya sheria hii ya kutoa huduma za utangaazaji katika vyombo vya habari. Kwenye sehemu ya pili ya sheria hii, yenyewe imeundwa na vifungu kuanzia cha tano (5) hadi cha 10, na kubwa zaidi lililopo ni pamoja na uanzishwaji wa Tume ya Utangaazaji Zanziba...

T.O.T WAPEWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA TABIANCHI

  Wanawake  wameombwa kuvitumia vyombo vya habari ipasavyo kwa lengo la kutangaza kazi wanazozifanya katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanawake viongozi  kupitia mradi wa ZanzAdapt Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa Ali amesema wanawake wanafanya mambo mengi katika jamii ila bado mchango wao haujatambulika kama ilivyo kwa wanaume hivyo kuvitumia vyombo vya habari kutawezesha kutambulika na kujitangaza kwa haraka hasa kupitia mitandao ya kijamii. Amesema historia ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla haioneshi mchango ama juhudi za wanawake kwa sababu wanawake bado hawajawa na ujasiri na uthubutu wa kutumia vyombo vya habari kwa usahihi. “Wanawake wanafanya mambo mengi katika jamii na kujitoa zaidi, sasa wakati umefika kueleza changamoto na mambo yanayowahusu kupitia vyombo vya habari ili kupatiwa ufumbuzi,” Dkt Mzuri. Mkufunzi katika mafunzo hayo Sophia Ngalapi amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya ...

KATIBU MKUU ABEDA ASAINI AGENDA YA MASUALA YA WANAWAKE KUHUSU AMANI, USALAMA

  NA MWANDISHI WETU, UNGUJA KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Abeida Rashid Abdallah amesaini Mpango wa Taifa wa kushughulikia Utekelezaji wa Agenda ya masuala ya Wanawake, kuhusu Amani na Usalama ulioandaliwa mahsusi kwa ajili ya kutekeleza Azimio Na:1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hafla ya utiaji saini imefanyika jana ofisini kwake Kinazini Unguja, amesema Mpango huo ni heshima kwa Tanzania kwani imeonesha wazi kukubali na kutekeleza Azimio hilo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha Wanawake wanakua  katika amani na usalama wakati wote. Amefahamisha kwamba Azimio hilo lilipitishwa tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2000, kwa lengo la kuhimiza umuhimu wa nafasi ya wanawake katika kuzuia na kutatua mizozo, mashauriano ya amani, ujenzi wa amani, ulinzi wa amani, hatua za usaidizi wa kibinadamu na ujenzi baada ya mizozo na kusisitiza umuhimu wa ushiriki sawa katika uendelezaji wa amani na usalama duniani. Ameeleza Wizara ya Maendeleo ya Jam...

MWAMBE MKOANI IN PEMBA ISLAND: CHILDREN FORCED TO A LIFE OF STONE CRUSHING

By HAJI NAASSOR, PEMBA@@@@   It is about an hour-and-a-quarter drive from Chake Chake town to Mwambe village in Mkoani District in the Southern Region of Pemba Island within Zanzibar country.   The village of Mwambe is located in a rocky area but is more fertile than the surrounding villages. It has three shehias, known here as Jombwe, Mwambe and Mchakwe.   The village has a population of 19,525,(2022 census) half of them children. Its people survive on agriculture growing beans for local consumption, and citrus and bananas to sell.   It has its own primary and secondary schools and a health centre that provides various medical services.   Besides, agriculture, the villagers are also engaged in fishing, stone crashing and mining. Since Mwambe is rocky, most people, especially the elderly and children, are involved in quarrying stone for sale.   The stone crashing business has forced many children to abandon school to earn money but this is taking its toll o...

VIFUNGU SHERIA YA TUME YA UTAANGAZAJI NAMAAJABU YAKE KUELEKEA UHURU WA HABARI ZANZIBAR

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ ZANZIBAR kama ilivyo eneo jingine lolote ulimwenguni, nayo inavyo vyombo vya habari, ambavyo maudhui yake ni sawa na vile vya mataifa mingine. Kazi za msingi za vyombo vya habari ni kuelemisha, kuburudisha na kuhabarisha ingawa kwa pia ni kukosoa, kupongeza na kuhoji. Kazi hii hasa ni haki ya kikatiba, katika nchi kadhaa, kwa mfano Zanzibar katiba yake ya mwaka 1984 kifungu cha 18 na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara 18 imeelezea haki hii. Kama hivyo ndivyo, unaweza kushangaa kuwa suala la kutoa, kupata na kusambaaza habari ni haki ya kikatiba, sasa iweje kutungwe sheria yenye vifungu au maneno, yenye ukakasi kwa waandishi wa habari. SHERIA YA TUME YA UTANGAAZAJI ZANZIBAR NO 7 YA MWAKA 1997 Sheria hii ambayo sasa inatimiza umri wa miaka 29, tokea pele ilipotiwa saini na Rais wa wakati huo wa Zanzibar Dk. Salmin Amour Juma, licha ya kufanyiwamarekebisho. Kwa hakika, lengo kuu la sheria hii, ni kuongoza vyombo vya habari Zanz...