Skip to main content

Posts

Showing posts from 2024

GROWING IN ADVERSITY: A STORY OF RESILIENCE FROM THE WOMEN OF UZI

  BY MUNIRA KAONEKA@@@@...... For many, the islands of Zanzibar evoke images of tropical forests and pristine beaches, and while that may be true , the very properties that make Zanzibar a unique tropical paradise also present significant challenging environments for its residents —particularly its farmers. Nearly half of the islands are occupied by coral terrain, characterized by a wide range of coral outcrops and soil patches in between, these geological features make  agriculture a demanding task, particularly for coastal communities such as those on Uzi Island. Situated to the south of Zanzibar's main island, Unguja, Uzi Island is a small community connected to the mainland by a causeway. The island’s coral bedrock dominates the landscape, leaving limited fertile ground for agriculture. What little arable land exists has been largely utilised for settlements, pushing farmers to adapt their practices and tools to the rugged coral terrain that remains. Traditional farming pr...

MICHEZO NI AFYA: WAZIRI PEMBE

NA MWANDISHI WETU, UNGUJA@@@@ W aziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kujiunga katika michezo mbali mbali ili kuimarisha afya zao pamoja na kuepukana na maradhi yasiyoambukiza. Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa uekaji jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa viwanja vya Michezo midogo midogo iitwayo "Michezo kwa Maendeleo (Sports for Development) katika viwanja vya Mwera Regeza Mwendo Wilaya ya Magharib A. Unguja. Waziri Pembe alifahamisha  kwamba hata viongozi wa dini na wataalumu wa Sekta ya Afya wamekua mstari wa mbele katika kuihamasiha jamii kufanya mazoezi au kujiingiza katika michezo mbali mbali ambapo hatua hiyo itasaidia kuimarisha afya na kuijiepusha na maradhi yasiyoambukiza ikiwemo kansa, kisukari na shindikizo la damu. Aidha alisema pia michezo ni ajira na sehemu ya kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hasa kwa vijana wa jinsia zote, kwani michezo inawasaidia kujiepusha na v...

ALI MBAROUK WA KONDE KUUKARIBISHA MWAKA MPYA AKIWA CHUO CHA MAFUNZO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa Wete, Zuwena Mohamed Abdul-kadir, amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne, mshitakiwa Ali Mbarouk Suleiman mwenye (18) mkaazi wa Konde Chanjaani, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuvunja nymba usiku na kuiba. Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung, yenye thamani ya shilingi 138,000 kwa kukisia mali ya Said Mohamed Salim. Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja nyumba usiku atatumikia  chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba simu atumikia kwa muda wa mwaka mmoja. Mbali na adhabu hiyo, pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mmiliki ambapo, hapo awali wakati wa kuiendesha kaesi hiyo, ilikua ni kielelezo cha ushahidi mahkamani hapo.  Mwendesha Mashtaka wa serikali Mohamed Ali Juma, alieleza kuwa kwa vile Mahkama imemuona na hatia mshitakiwa huyo, ni vyema kutoa adha...

HABARI KAMILI YA POLISI PEMBA ANAYEDAIWA KUBAKA AKIWA KITUONI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, limekiri kupokea malalamiko ya mwanamke mmoja, akimtuhumu mtendaji wa Jeshi hilo, kumbaka ndani ya kituo cha Polisi. Jeshi hilo limesema, ni kweli walipokea lalalamiko hilo, ingawa lilisema ili kukamilisha na kutoa taarifa rasmi, wamo kwenye upelelezi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Disemba 6 mwaka huu majira ya saa 8: 17, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mussa Mwakasula, alisema kwa sasa hawana taarifa pana  juu ya tukio hilo. Alieleza kuwa, kwa sasa wanaendelea na uchunguuzi wa tukio hilo, na hasa baada ya kuzipata taarifa hizo, kutoka kwa mlalamikaji. ‘’Ni kweli tumepokea lalamiko la mwanamke mmoja, akimtaja askari wetu, kwamba ndie aliyembaka, ingawa kwa sasa taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguuzi wetu kukamilika,’’alisema Kaimu Kamanda huyo. Baadhi ya wananchi waliokataa kutaja majina yao , walisema mwanamke huyo kabla ya kudai kutendewa kosa hilo, alifika kituo cha Poli...

CFP EMPOWERS AGROFORESTRY FARMERS WITH WATER SOLUTIONS

BY KHELEF NASSOR, ZANZIBAR IN a significant stride towards sustainable agriculture, Community Forests Pemba-CFP recently distributed essential water materials to agroforestry farmers in four shehias of Uzi, N'gambwa, Unguja Ukuu, and Bungi. This generous initiative, part of the ZanzAdapt project funded by Global Affairs Canada, aims to address the persistent water scarcity challenge faced by many Agroforestry farmers in the target areas of the project implementation. The distribution ceremony conducted at Uzi shehia, graced by the presence of the Regional Commissioner of South Unguja, Hon. Ayoub Mohammed Mahmoud, marked a pivotal moment for the local farming community. The event also saw participation from the Principal Secretary of the Ministry of Agriculture, Ali Khamis Juma, who expressed the ministry's commitment to collaborating with CFP in fostering sustainable agricultural practices. The distributed water materials, including solar system, water tanks, water pumps, subme...

SHERIA ZA UCHAGUZI ZANZIBAR : JE, ZINAWEZESHA AU ZINAKWAMISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KWENYE SIASA?

    Na Nusra Shaaban Ushiriki wa wanawake katika siasa ni moja ya hatua muhimu katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu.  Lakini Zanzibar, ambapo wanawake wanaunda zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura, idadi yao kwenye nafasi za uongozi bado ni ndogo. Takwimu za mwaka 2020 zinaonyesha kwamba wanawake walichangia asilimia 22 tu ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Je, sheria za uchaguzi zina mchango gani katika hali hii? Changamoto Zinazowakabili Wanawake Katika Siasa Mifumo ya uchaguzi Zanzibar imekuwa ikibeba changamoto mbalimbali kwa wanawake wanaotaka kushiriki siasa. Kwa mujibu wa Hidaya Yussuph Ali, Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo, mfumo wa kura ya mapema umekuwa ni kikwazo kikubwa. "Wanawake wanakata tamaa kwa sababu mfumo huu unatoa mianya ya rushwa na udanganyifu, huku ukiongeza gharama kwa wagombea wanawake," anasema. Gharama za kugombea pia zimekuwa mzigo mkubwa kwa wanawake wengi. Mtumwa Faiz Sadiki, Naibu Katibu Mkuu wa ADC, anael...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...

TAMWA-ZANZIBAR: 'WAANDISHI PIGIENI DEBE HADI IPATIKANE SHERIA MPYA YA HABARI'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wametakiwa kuendelea kutilia mkazo, suala la upatikanaji wa sheria mpya na rafiki ya habari Zanzibar Hayo yameelezwa Disemba 9, 2024 Afisa Program na mchechemuzi wa mpitio za sheria za habari Zanzibar, kutoka TAMWA-Zanzibar Zaina Abdulla Mzee, alipokuwa akifungua mafunzo ya ukumbusho wa sheria hizo, kwa waandishi wa habari wa Pemba, yaliofanyika ofisi ya TAMWA-Pemba. Alieleza kuwa, waandishi wa habari ndio wahusika wakuu wa sheria hiyo, hivyo wanaowajibu wa kupigia debe na kuandika juu ya madhara yaliopo kwenye sheria zilizopo. Alisema, mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya, umekuwa ukionekana kwa mwendo wa kusua sua, hivyo waandishi wa habari, wanaweza kutumia kalamu zao, kuchapuza mchakato huo. ‘’Waandishi wa habari, mnaweza kuchapuza kwa haraka mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya, kwa kutumia vipindi na makala mbali mbali, zinazoelezea changamoto za sheria zinazitumika sasa,’’alisema. Akiwasilisha vifungu cha sh...

JAMII YATAKIWA KUZIDISHA KASI MAPAMBANO YA UDHALILISHAJI, UKATILI

NA MWANDISHI MAALUM, PEMBA JAMII imetakiwa kuendelea kushirikishiana katika kupinga ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa wanawake na watoto nchini, ili kuondosha vitendo hivyo. Wito huo umetolewa na mweyekiti wa Madiwani Baraza mji Mkoani Mohamed Said Ali akifunguwa kongamano la kujadili ukatili kijinsia kwa wanafunzi na wanajamii wa mkoani liloandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za wanawake Tanzania kisiwani Pemba ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani. Amesema serekali inaendelea kuchukuwa jitihada mbali mbali za upinga vitendo hivyo ikiwemo kuwachukulia hatuwa za kisheria watendaji wa makosa hao. Aidha amesema licha jitihada hizo lakin bado kuna baadhi ya Jamii wanakwamisha jitihada hizo kwa kutotowa tarifa za ukatili kwa vyombo vya sheria kuchukuliwa hatuwa na badala yake kuzimaliza wenywe majumbani au kutotowa ushahidi wa katika vyombo vya sheria. "Serekali inajitahidi kupambana kuona vitendo hivi vinaondoka lakin Hadi sasa Kuna b...

MKURUGENZI TUJIPE: ‘ELIMU KIDATO CHA NNE BADO NDOGO JIENDELEZENI'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAHITIMU kidato cha nne skuli ya sekondari Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wamekumbushwa kuwa, elimu waliyoipata bado ni ndogo, hasa kwa ulimwengu ulivyo, na badala yake, watafute namna ya kujiendeleza. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellem, kwenye mahafali ya 18 ya wanafunzi hao, yaliofanyika skulini hapo. Aliwaambia wahitimu hao kuwa, kwa sasa elimu imeongezeka thamani, na ndio maana kidato cha nne ni kama mwanzo wa kutafuta elimu, hivyo wahakikishe wanashirikiana na familia zao, ili kujisomea zaidi. Alieleza kuwa, kwa sasa kuanzia kidato cha sita na kuendelea, ndio mwanzo wa elimu, hivyo kwa wale wanafunzi ambao hatobahatika kuendelea kidato cha tano na sita, wasivunjike moyo. ‘’Elimu ya kidato cha nne, kama ndio mwanzo wa elimu kwa dunia ya sasa, na wale ambao hawatobahatika, bado nafasi ya kujiendeleza kimasomo wanayo,’’aliwakumbusha. Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ‘TUJIPE’ aliwasisit...